Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 11 August 2017

RAIS WA FATTAH EL-SISI WA MISRI KUWASILI NCHINI JUMATATU HII

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi  anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu Agosti 14, mwaka huu  kwaajili ya ziara ya siku mbili ambapo ataongozana na ujumbe wake na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli.

Kutokana na ugeni huo mzito Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam ikiwemo wenye Hotel, Magari na Migahawa kuchangamkia fursa ya ugeni huo katika kufanya biashara ili kujipatia kipato na kukuza Biashara zao.

Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kuonyesha ukarimu tangu Rais atakapowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere hadi hapo atakaporejea nchini Misri siku ya Jumanne.

Ugeni huu ni matunda ya uwezo wa Rais Magufuli katika kujenga  mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali ulimwenguni.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment