Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 11 August 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAELEZORAIS Dk. John Magufuli amemteua Dk. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa uteuzi wa Dk. Abbas ulianza tangu   Agosti 9, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002.

Dk. Abbas ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, ambapo nafasi hiyo imebadilishwa kutoka Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya uteuzi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment