Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 25 August 2017

MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE

Mahujaji kutoka sehemu mbalimbali nchini takribani 100 ambao wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam kwenda hija wakiwa uwanjani hapo usiku huu pasipo kujua hatma ya safari yao hiyo ya kwenda kutimiza ibada ya Hija, katika Mtakatifu wa Makkah, Saud Arabia baada ya kudai kutapeliwa na waliokuwa wakiratibu safari yao kupitia taasisi za  Taiba Hajj & Umrah Social Service Trust na Jamarat Hajj and Umrah Traveller (Picha na Katuma Masamba).
Mahujaji kutoka sehemu mbalimbali nchini takribani 100 ambao wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam kwenda hija wakiwa uwanjani hapo usiku huu pasipo kujua hatma ya safari yao hiyo ya kwenda kutimiza ibada ya Hija, katika Mtakatifu wa Makkah, Saud Arabia baada ya kudai kutapeliwa na waliokuwa wakiratibu safari yao kupitia taasisi za Taiba Hajj & Umrah Social Service Trust na Jamarat Hajj and Umrah Traveller
MAHUJAJI takribani 100 wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jiji Dar es Salaam  kwenda kufanya Hijja katika mji Mtakatifu wa Makka kutokana na taasisi zilizotakiwa kuwasafirishwa kushindwa kufanya hivyo. Anaandika Katuma Masamba.

Mahujaji hao ambao walitakiwa kuondoka leo wameshindwa kuondoka baada ya kuwepo sintofahamu huku viongozi wa Taasisi ya Taiba Hajj & Umrah Social Service Trust na Jamarat Hajj and Umrah Traveller hali iliyowafanya mahujaji hao kutofahamu hatma yao.

Akizungumza na TSN Digital uwanja hapa, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir  amewataka Mahujaji hao kuwa na subira wakati wakitafuta namna ya wao kuweza kusafiri ka ajili ya kwenda kutekeleza Ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika Nguzo za Kiislamu.

"Kipindi hiki mpaka kesho tunatarajia kupata majibu yoyote kutokana juhudi za viongozi, naomba mstahamili  tufanye subira tuone tutafikia wapi...mimi nitaendelea kufuatilia kuona safari inakamilika kiasi gani kupitia viongozi, kuna wengine hatujawapata hadi sasa lakini tunawatafuta," amesema Mufti.

Aidha, amewatoa hofu Mahujaji hao kuwa mipaka ya Mji wa Makka kufungwa usiku wa kuamkia Jumapili, hivyo muda bado upo wa kuweza kupata safari na kuwataka mahujaji hao kufanya dua na kumuomba Mungu ili waweze kutekeleze ibada hiyo.

Akizungumzia hatua ya kutekelezwa uwanjani hapo, Hussein Said Seif ambaye ametokea mkoani Mwanza amesema alilipa Sh milioni 8.5 kwa taasisi ta Taibah ili aweze kutekeleza ibada hiyo lakini hadi usiku hakuna jambo linaloeleweka ambapo ameshauri serikali kuchukua hatua dhidi ya taasisi za aina hiyo.

Naye, Ummy Sekibo  mkazi wa Dar es Salaam amesema, hali imewasikitisha wananchi na waislamu wote kwa ujumla kwani kitendo hicho si jambo jema na kwamba taasisi hiyo inapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo ya kufutiwa usajili wake.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment