Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 11 July 2017

WAZIRI MWIGULU MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, MJINI DODOMA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, anataraji kufungua Mkutano wa Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara utakaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF, mjini Dodoma.

Mkutano huo wa siku mbili utakaofanyika Julai 13 na 14 ndio Kikao cha juu cha Jeshi ambacho huwahusisha Makamanda wa Mikoa yote ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu na Wakuu wa Vitengo vyote vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Kauli mbiu ya Mkutano wa huo ni “KUOKOA MAISHA NA MALI NI WAJIBU WETU ILI KULETA MAENDELEO YA TAIFA, ZINGATIA UTOAJI HUDUMA WENYE MAADILI NA UADILIFU ILI KULETA TIJA”

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ASF. Puyo Nzalayaimisi  ilisema Mkutano huo wa mwaka unalenga kutathimini kwa pamoja utendaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika maeneo yake yote na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo, kurekebisha dosari zilizojitokeza na kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji kazi kwa ujumla katika mwaka unaofuata.

Nzalayaimisi alisema mada kuu ya Mkutano  huo itatolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye ambapo mada hiyo itaendana na dhana nzima ya Sera na Dira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Aidha Maamuzi na mikakati mbalimbali itakayotolewa na Mkutano huu itakuwa na umuhimu wa pekee katika kuandaa na kutoa miongozo mbalimbali ya utendaji katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hili kama dira inavyosema kuongoza katika utoaji huduma bora ifikapo mwaka 2025.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment