Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 11 July 2017

RC MBEYA AZINDUA UWEKAJI ALAMA MIFUGO


 Mkuu wa  Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akizindua uwekaji alama mifugo katika Kijiji cha Soweto wilayani Chunya mkoani Mbeya leo.
MKUU wa  Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amezindua uwekaji alama mifugo mkoani Mbeya.

Makalla amefanya uzinduzi huo leo katika Kijiji cha Soweto wilayani Chunya na kusema kuwa uwekaji alama mifugo ni utekelezaji wa sheria ya mifugo namba 12 ya mwaka 2010.

Amewataka wafugaji wote 2,755 wa Wilayani Chunya kuhakikisha kuwa Ng’ombe 282,517 wanawasajili na kupiga chapa.

Makalla amesema faida ya kusajili na kuweka alama mifugo kuwa ni pamoja na kujua idadi ya mifugo, kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Aidha amesema kuwa faida nyingine ni kuzuia uingiaji mifugo kiholela na kuthibiti magonjwa ya  mifugo.

Amekiagiza kikosi kazi kinachofanya kazi hiyo kuhakkisha kinakamilisha uwekaji alama mifugo katika kipindi cha mwezi mmoja.

Amewapongeza wafugaji kujitokeza kwa wingi na hii ni kutokana na maandalizi mazuri ikiwemo Elimu ya kutosha kabla ya zoezi kuanza.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment