Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akishiriki dua ya kumuombea
marehemu ya aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani
kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha
maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan
Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, akisaini kitabu cha maombolezo, katika
msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani
kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu
Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, wakati akiwasili kwenye msiba wa aliyekua Karani
wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala
Majimatitu, (katikati) ni Katibu Mkuu Ikulu Alphayo Kidata, Julai 7, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitoa pole kwa niaba ya
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza
la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai
7, 2017.
********************
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi
kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan
Shebuge.
Marehemu
Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala-
Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi,
Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Bw.
Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya
kupata na shinikizo la damu.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali.
Amesema
enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na
kutoa mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa
majukumu ya Serikali kwa ufanisi.
“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”
Awali,
Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw.
Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.
Alisema
marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia
mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika
shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani
Tanga.
Bw.
Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya
Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha
sita.
Alisema
mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada
ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya
uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo
mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment