Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 7 June 2017

WAHASIBU HALMASHAURI MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA KATI WAFUNDISHWA MFUMO WA KIELEKRONIKI KUJAZA TAARIFA ZA FEDHA

Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akielezea kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Bwana Elizeus Rwezaula akizungumza ukumbini


Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza ukumbini ambapo alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kielektroniki ulibuniwa na PS3 kisha kuwasiliana na serikali ambayo kwa pamoja wameamua kutekeleza mfumo huo katika halmashauri mbalimbali nchini 
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akijifunza kwa vitendo jinsi ya kuingiza taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki
Washiriki wa mafunzo hayo wakijifunza kwa vitendo namna ya kujaza taarifa za fedha kwa kutumia kompyuta
Mwenyekiti wa mafunzo hayo ya FFARS ,Samson William akizungumza ukumbini wakati akiendesha majadiliano mbalimbali

Mkuu wa  Kitengo cha Habari na Mawasiliano PS3, Leah Mwainyekule akielezea utaratibu utakaotumika kwa wakufunzi waliopata mafunzo ya FFARS watakavyokwenda kutoka elimu kuhusu FFARS katika vituo vya kutolea huduma

Kabla ya kufundishwa njia ya kieletroniki katika kujaza taarifa za fedha,washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika kikundi wakijadili namna ya kujaza taarifa kwa njia ya zamani ya kutumia vitabu.Walijadili namna ya kutunza kumbukumbu za miamala ya kifedha na nyaraka kwa kutumia vitabu
Washiriki wakiendelea na kazi ya vikundi.Washiriki hao walijifunza pia namna ya kuandika miamala ya kifedha kwenye nyaraka na vitabu vya uhasibu. Picha na Kadama Malunde Blog.
********************
WAHASIBU zaidi ya 130 kutoka Halmashauri za Wilaya kutoka  mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati wameanza kupatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki kuhusu Usimamizi wa fedha ngazi za msingi zikiwemo Zahanati,vituo vya Afya,Hospitali na Shule za Msingi na Sekondari.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System’ ( FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1,2017 katika halmashauri mbalimbali nchini.

Wahasibu hao wanashiriki katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3,TAMISEMI,Wizara ya afya,wizara ya elimu.

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma unasaidia kurahisisha kazi.

“Katika Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo nchi pekee itakayoanza kutumia mfumo huu wa kisasa wa kielektroniki katika uingizaji taarifa za fedha katika ngazi za msingi za kutolea huduma,na umetengezwa na vijana wa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) unafanikiwa”,alieleza Rwezaula.

“Tunawashauri wale wanaoendelea kutumia mfumo wa zamani wa ujazaji taarifa kwa kutumia vitabu (manual) waanze kutumia mfumo huu mpya wa uingizaji taarifa kwa mfumo wa kompyuta ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia”,aliongeza Rwezaula.

Kwa upande Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dk. Suma Kaare alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kieletroniki ulipendekezwa na PS3 na tayari serikali imeukubali na utaanza kutekeleza mwezi Julai,2017 katika halmashauri mbalimbali.

Naye Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago alisema baada ya wahasibu hao kupatiwa mafunzo kuhufu FFARS nao wataenda kutoa elimu kuhusu mfumo kwa watoa huduma wengine wa ngazi za chini.

Mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) yamemalizika leo mjini Shinyanga.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment