Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 7 June 2017

SHULE YA SEKONDARI BARABARA YA MWINYI DAR ES SALAAM YAFANYIWA UKARABATI

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick wakifurahia baada ya kuzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa shule hiyo, Sostenes Nyenyembe (kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.
Sehemu ya Madarasa na eneo lililofanyiwa ukarabati na kampuni ya Bam International Africa.
Sehemu ya Madarasa na eneo lililofanyiwa ukarabati na kampuni ya Bam International Africa.Na Robert Okanda Blogspot
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akiwatembeza wageni kujionea ukamilishwaji wa mradi wa ukarabati wa madarasa na ujenzi wa eneo la makusanyiko kabla ya kufanya uzinduzi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Barabara ya Mwinyi alipotembelea mojawapo ya madarasa matano, kampuni hiyo iliyoyakarabati eneo la Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa
Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick kulia akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla alipokuwa akikagua mazingira ya Shule hiyo.
Juu na chini, Baadhi ya wanafunzi wakionesha umahiri wa kucheza 'Martial Arts' kunogesha hafla hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akifanya utambulisho wa walimu wa shule kwa wageni.
Wanafunzi nao wakitambulishwa.
Waalimu wa shule hiyo wakimtambulishwa kwa wageni na viongozi.
Meneja Maendeleo ya Biashara, Kampuni ya Bam International, Noreen Mazalla akimtambulisha Meneja Ubora kwa Afrika wa kampuni hiyo, Lily Naah.
Meneja Maendeleo ya Biashara, Kampuni ya Bam International, Noreen Mazalla akimtambulisha Afisa usalama wa kampuni hiyo.
Skauti wa shule hiyo wakipandisha bendera ya Bam International kwenye shule yao
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick (aliyevaa miwani), Mwenyekiti wa shule, Sostenes Nyenyembe (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa, Noreen Mazalla na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa (kushoto) baada ya kuzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017.
 Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bam International wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo.
Mwalimu akisoma risala.
Wanafunzi wakiimba shairi la kuwashukuru viongozi wa kampuni hiyo.
Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akizngumza machache na wanafunzi wa shule hiyo.
Wanafunzi wakiaga kwa madaa baada kuimba shairi la shukrani kwa viongozi wa kampuni hiyo.
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick.

Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick na Meneja Maendeleo ya Biashara, Noreen Mazalla wakipanda mti wa ukumbusho katika eneo la makusanyiko la shule hiyo uliofanywa kampuni hiyo katika shule ya Barabara ya Mwinyi Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Eric Kilangwa (wa tatu kushoto) na Mwenyekiti wa shule hiyo Sostenes Nyenyembe.
Picha ya pamoja viongozi wa Bam International, Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam. 


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment