BUNGE limetoa waraka namba mbili kwa ajili ya kuunda
kamati maalum ya wabunge tisa watakaochunguza mwenendo mzima wa madini ya
Tanzanianite ili kuona namna madini hayo yanavyonufaisha watanzania.Anaandika Halima Mlacha kutoka Bungeni Dodoma.
Wabunge walioteuliwa kuwa katika kamati hiyo
kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dotto Biteko,
mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa (CCM), mbunge wa Msalala Ezekiel Maige
(CCM) na mbunge wa Muheza Balozi Adadi Rajabu (CCM).
Wabunge wengine ni mbunge wa Viti Maalum, Mary
Mwanjelwa (CCM), mbunge wa vitimaalum Subira Mgalu (CCM), mbunge wa Ole Juma
Hamad Omar (CUF), mbunge wa viti maalum Lathifa Chande (Chadema) na mbunge wa
Simanjiro James Millya (Chadema).
Alitaja hadidu rejea za kamati hiyo maalum kuwa ni
kupitia mkataba uliopo baina ya Shirika la Madini la taifa (Stamico) na kampuni
ya Tanzanite One minning na kuangalia ushiriki wa Sky Associate ili kuona
manufaa ambayo nchi inapata kutokana na madini hayo ambayo ni ghali zaidi
duniani.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment