RAIS wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amesema watafanya marekebisho
ya kanuni za soka ili ziendane na zile za Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Malinzi
aliyasema hayo wakati akitoa shukrani kwa Rais na uongozi wa Serikali na watanzania
kwa jinsi walivyoiunga mkono timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17
‘Serengeti boys’ iliyoshiriki Fainali za 12 za Vijana zilizofanyika nchini
Gabon kuanzia Mei 14-28.
Akizungumza
kwa hisia Malinzi alisema Serengeti boys iliondolewa kwenye mashindano katika
hatua ya makundi kwa kipegele cha kuangalia mchezo mliokutana nani alimfunga
(head to head) mwingine akaahidi kubadili kanuni ili ziendane na kanuni za CAF.
“Kanuni
ilitumika kuiondoa Serengeti boys kwenye mashindano tungekuwa tunaitumia hapa
kwetu basi Simba angekuwa bingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2016/2017,” alisema
Malinzi.
Pia Malinzi
alisema watashusha mashindano ya U-20 kuwa ya wachezaji wa U-17 ili kusaidia
kupatikana kwa timu za vijana imara wanaotokea kwenye klabu kuliko ilivyo sasa
TFF ndio inakuwa na jukumu la kuandaa timu za vijana.
Serengeti
boys katika mashindano ya AFCON U-17 ilikuwa kundi B pamoja na timu za Mali,
Angola na Niger lakini ikaondolewa na Niger.
Katika
mchezo wa awali Serengeti boys ilitoka suluhu na Mali, ikaifunga Angola mabao
2-1 na kufungwa na Niger bao 1-0.
Endapo TFF
ilikuwa inatumia kanuni hiyo basi Simba ingekuwa bingwa kwani baada ya ligi
kumalizika Simba na Yanga zilikuwa sawa kwa pointi 68 lakini ingefaidika kwani
mchezo wa awali ilitoka sare ya 1-1 na raundi ya pili Simba ikashinda mabao
2-0.
Malinzi
alisema anaamini kamati ya utendaji itakubali kupitisha kipengele hicho ili
kuanzia msimu ujao zitumike kwenye ligi zote za TFF.
Aidha
Malinzi alisema Serengeti boys itakuwa ndio timu ya U-20 ‘Ngorongoro Heroes’
ambayo zitafanyika 2019 hivyo benchi la Ufundi litaanza kambi za maandalizi kwa
kucheza michezo za majaribio za nje ya nchi na ndani.
Pia Malinzi
aliipongeza Zambia kwa kufuzu robo fainali ya mashindano ya Vijana ya dunia ya
U-20 yanayofanyika Korea Kusini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment