NA
IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU
wa NEC, Idara ya Organazesheni ya CCM
Taifa, Nd. Pereira Ame Silima amewataka viongozi na watendaji wanaochaguliwa
kwenye uchaguzi wa chama na jumuiya zake kwa sasa kuwa na fikra na
mitizamo mipya itakayoongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya CCM.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati za siasa za Mikoa ya
CCM Mjini na Magharibi pamoja na wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji
za jumuiya za Chama hicho huko Amani Unguja, alisema chama hicho kitaendelea
kuwa imara kutokana na utamaduni wa kupata viongozi kwa njia za kidemokrasia
hasa Uchaguzi huru na wa haki.
Alisema
lengo la ziara hiyo ni kuimarisha chama sambamba na kujitambulisha kwa
viongozi hao kwani tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni
Mjini Dodoma hiyo ndio ziara yake ya mwanzo.
Alizitaka
kamati mbali mbali zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuchuja viongozi katika uchaguzi wa chama hicho kuhakikisha
wanapatikana viongozi wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji
ndani ya chama hicho na sio wababaishaji.
Aidha
Katibu huyo alisema Chama hicho kina nia ya kuanzisha utaratibu wa kutengeneza
kadi za uanachama zitakazokuwa katika mfumo wa kielectroniki ili kupata idadi
kamili ya wanachama kwa lengo la kujipanga katika michakato ya uchaguzi wa
ndani na wa Dola.
“
Viongozi na watendaji wenzangu tujue kuwa chama cha mapinduzi kipo kwa ajili ya
wananchi wote hivyo lazima tufanye kazi kwa ushirikiano ili tutimize kwa
vitendo dhamira ya mabadiliko yaliyofanywa ndani ya Katiba yanayolenga kuongeza
ufanisi katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiuchumi ndani ya chama chetu.”,
alisema Katibu Amen a kuongeza kuwa dhana
ya CCM mpya itekelezwe na kusimamiwa na fikra mpya na sio upya wa viongozi
wanaochaguliwa kwa sasa.
Alisisitiza
umuhimu wa kufuata Katiba kwa kila
hatua ya kufanya maamuzi ndani ya chama
hicho kwa lengo la kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya lazima kwa baadhi ya
wanachama wanaokwenda kinyume na maadili ya Chama hicho.
Hata
hivyo aliyataja majukumu muhimu yanayotakiwa kutekelezwa na idara yake kuwa ni
kusimamia Uchaguzi wa Chama na Dola pamoja na kusimamia jumuiya za CCM kuhakikisha
zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa miongozo ya Kikatiba.
Mapema
akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Bora Afya Silima
Juma alisema Mkoa huo unaendelea kupanga
mikakati ya kudumu itakayosaidia chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akisoma
taarifa ya utekelezaji Katibu wa CCM Mkoa wa
Magharibi, Aziza Ramadhan Mapuri alisema licha ya kuwepo kwa changamoto
ndogo ndogo katika uchaguzi unaoendea hivi sasa ndani ya mkoa huo wamefanikiwa
kuwapata viongozi makini na wachapaka kwa baadhi ya ngazi ambazo tayari
zimeshakamilisha zoezi hilo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment