Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 2 June 2017

MBUNGE WA KIBAMBA JOHN MNYIKA ATOLEWA NJE YA BUNGE LEO

MBUNGE  wa Jimbo la Kibamba na Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, John Mnyika atolewa kinguvu na askari wa Bunge kuafuatia amri ya Spika wa Bunge Job Ndugai hii leo kwa kile kilochoelezwa kuwa ni utovu nidhamu kwa Mbunge huyo kujibizana na Mbunge mwenzake bila kufuata utaratibu wa kiti ndipo Spika akaamuru atolewe nje.
Inadaiwa kuwa Mbunge huyo wa Kibamba, John Mnyika alikuwa akijibizana na Mbunge Livingstone Lisinde na kuonywa mara kadhaa na Spika Job Ndugai ili afuate utaratibu lakini akawa anaendelea kujibizana ndipo alipoamrisha askari wamtoe nje kwa nguvu.
 Wabunge mbalimbali wa Kambi rasmi ya Upinzani  Bungeni wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiunga mkono mwenzao John Mnyika kutolewa. Wabunge wa Chadema, Ester Bulaya wa Bunda Mjini na Halima Mdee wa Kawe  nao wameingia matatanani kufuatia sakata hilo na Spika ameiagiza Kamati ya Bunge ya Maadili kuwahoji na kupendekeza adhabu. 

Itakumbukwa hivi Karibuni Halima Mdee alisamehewa na Bunge kwa kudharau kiti cha Spika na kutakiwa kutofanya kosa lingine lolote la kudharau mamlaka ya Spika na kufanya kosa lingine lolote la uvunjifu wa kanuni za kudumu za Bunge, utekelezaji wa adhabu uanze mara moja kwa maelekezo ya kiti cha Spika.
 Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutoka nje.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini (CUF) Maftaha Nachuma akiwa peke yake amebaki Bungeni baada ya wenzake wa kambi ya upinzani Bungeni kutoka nje leo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment