TAASISI ya Nathan Mpangala NMF
itaendesha warsha ya siku tatu itakayofanyika katika ukumbi wa Nafasi
Art Space, Dar es Salaam inakusudia kuwajengea uwezo wachora vibonzo
vijana ambao tayari wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari na wale
ambao bado hawajapata nafasi hiyo.
Kutokana na mabadiliko ya
teknolojia duniani, NMF inaamini kuwa kuna umuhimu wa wachora vibonzo
wakapata mafunzo ya mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko hayo.
Mwenyekiti wa NMF, Nathan Mpangala amesema kuwa warsha hiyo itafanyika Juni 7-9 mwaka huu na itafuatiwa na
onesho la wazi la vibonzo vilivyochorwa katika warsha hiyo siku ya
Jumamosi, tarehe 10/6/2017 kuanzia saa 10.00 alasiri mpaka 12 jioni
katika katika ukumbi huo huo ambapo wakaazi mbalimbali wanakaribishwa.
Hakutakuwa na kiingilio.
Mpangala alisema,
NMF inayoamini kuwa kipaji
kinakuwa na maana pale tu kinapoibuliwa, endelezwa, nufaisha msanii na
Taifa, inatoa shukrani kwa Ubalozi wa Uswis nchini Tanzania, Nafasi Art
Space na RUKA Kipro kwa kuwezesha warsha hii kufanyika.
NMF inatoa wito kwa wadau
mbalimbali kuiunga mkono hasa katika eneo la kuwajengea uwezo vijana
wenye ndoto ya kuja kuwa wasanii hodari nchini.
Nathan Mpangala Foundation (NMF),
No.5286, yenye makao yake jijini Dar es Salaam, ni asasi isiyokuwa ya
kiserikali iliyosajiliwa mwishoni mwa mwaka jana kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi
na Udhamini (RITA) ikiwa na malengo kadhaa ikiwemo mafunzo ya sanaa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment