Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 21 June 2017

MARA YAANZA VYEMA MPIRA WA KENGELE

Kocha mkuu wa mkoa wa Mara Saddy Omary ameipongeza timu yake ya mchezo wa mpira wa kengele ya wasichana kwa kuanza vyema mashindano ya michezo ya shule msingi nchini(UMITASHUMTA).

Kocha Saddy alisema ana imani timu yake itafanya vyema kuhakikisha inafika hatua ya fainali na kuchukua ubingwa.

Timu ya Mara ilishinda kwa mabao 14-12 dhidi ya Manyara.Saddy alisema mchezo wa mpira wa Kengele nchini una changamoto nyingi sana na wadau wamekuwa hawatoi kipaumbele kwajili ya mchezo huo.

Saddy alisema changamoto nyingine wanayopata katika kuendeleza mchezo huo ni gharama ya vifaa kwajili ya mchezo huo,ikiwemo mpira wa mchezo huo ambapo unauzwa 300,000/-.

Saddy anaiomba chama cha mchezo huo kwa walemavu wasioona(TBSA) kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa jamii kuhusiana na mchezo huo.

Kocha Omary alisema serikali iendelee kutoa mafunzo ya kutosha kwa walimu wa mchezo huo nchini.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment