Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya kuchunguza mchanga wa madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi (Makinikia) Prof. Nehemia Osoro akiwasilisha ripoti yake kwa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
******************
KAMATI ya Pili ya uchunguzi wa mchanga wenye madini imependekeza serikali kupitia
Msajili wa Makampuni kuichukulia hatua kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia
Mine PL Cambayo imekuwa ikiendesha shughuli zake kinyume cha sheria. Anaandika Katuka Masamba-dailynewstzonline.blog.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Nehemia Osoro amesema, wamebaini kuwa kampuni
hiyo haijasajiliwa katika taasisi yoyote nchini.
Aidha, kamati hiyo imependekeza serikali kuzuia usafirishaji wa makinikia,
hadi hapo wadaiwa watakapolipa madeni yao yote na pia kuwachukulia hatua
waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Manaibu na watumishi wote
waliohusika katika upotevu wa mapato.
Kamati hiyo pia imependekeza, serikali ianzishe utaratibu utakaowezesha
ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeza
ajira kwa Watanzania.
“Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya migodi na viwanja vya
ndege vilivyoko migodini ili kudhibiti vitendo vya hujuma zinazoweza kufanywa
na baadhi ya makampuni za madini,” amesema Profesa Osoro wakati akisoma
mapendekezo ya kamati hiyo.
Mapendekezo mengine yaliyowasilishwa na kamati hiyo ni, Sheria iweke kiwango
maalumu ya kiwango cha hisa ambacho kitamilikiwa na serikali katika makampuni
zote za madini, serikali ichunguze mwenendo wa watumishi wa Mabaraza ya Kodi
kwa kuchukua muda mrefu kutoa maamuzi ya mashauri ya kodi.
Sheria itamke bayana kuwa madini ni maliasi asili ya Watanzania na iwekwe
chini ya uangalizi wa Rais kwa manufaa ya Watanzania. Sheria ielekeze makampuni
ya madini ziweke fedha zinazotokana na mauzo yao katika mabenki ya nchini ili
kukuza uchumi wa nchi na kuondoa mianya ya ukwepoaji kodi
Profesa Osoro aliongeza kuwa, mikataba ya madini isiwe ya siri na ni lazima
iridhiwe na bunge na pia serikali itoe elimu kwa watumishi wake kuhusu sekta ya
madini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment