Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana
na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua
ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa
maelekezo Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya
upandaji nyasi kwenye eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa
barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka
kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya
Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa Arumeru
Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa
wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari
juu ya gema lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi
wa daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei
4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment