Mwanasheria wa NEMC Benard Kongola (kulia) akiandika maelezo ya bw
Athanas Mushi meneja wa shamba la Tommy Diaries Farm.
**********
Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC)
limeyatoza faini mashamba ya mifugo ya Tommy na Ndoto jumla ya shilingi milioni
20 kutokana na kukiuka Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
Faini
hizo zilitangazwa na wakili wa serikali mkuu kutoka NEMC, Benard Kongola baada
ya kikosi kazi namba tatu cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha mkuu kukagua hali
ya uhifadhi wa mazingira katika mashamba ya mifugo ya Tommy na Ndoto yaliyopo
wilayani Kilolo Mkoani Iringa jana.
Baada
ya kitamka faini hizo, wakili Kongola alisema kuwa Shamba la mifugo la Tommy
limetozwa faini kutokana na kulima mahindi na migomba ndani ya mita 60 kutoka
ukingo wa mto Ruaha mdogo. Alisema kuwa shamba la mifugo la Ndoto limetozwa
faini kutokana na kufanya biashara bila kuwa na cheti ya tathmini ya hali ya
mazingira kutoka NEMC.
Wakili
Kongola alisema kuwa faini hizo zinatakiwa kuwa zimelipwa ndani ya siku 14 toka
tarehe ya faini hiyo. Aliongeza kuwa baada ya siku 14 NEMC wataenda kukagua
utekelezaji wa agizo hilo.
Kikosi
kazi hicho kikiwa katika ukaguzi wa hali ya uharibifu wa mazingira katika
shamba la mifugo la Tommy kilibaini uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na
kupandwa miti isiyo rafiki kwa mazingira na kusababisha kukauka kwa vyanzo vya
maji.
Mwenyekiti
wa kikosi kazi hicho ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu
alisema “chanzo hiki cha maji ambacho
kinaelekea kukauka lazima kihifadhiwe ili kirudie hali yake ya awali. Miti hii yote
ambayo si rafiki kwa mazingira lazima ikatwe na kupandwa miti ambayo ni rafiki
kwa maji na niletewe taarifa ya utekelezaji ndani ya wiki moja, alisema Ayubu”.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment