Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 27 April 2017

KIKOSIKAZI CHA MAKAMU WA RAIS CHATEMBELEA MBARALI

Wajumbe wa Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha (kikundi namba 2) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisubiri kupanda boti ya upepo ili kutembelea eneo la bonde la Ihefu lililoko Mbalari- Mkoani Mbeya kugagua ikolojia ya Bonde hilo.



Wajumbe wa Kikosi kazi wakiwa ndani ya boti katikakti ya bonde la Ihefu wakiakagua ikolojia ya bonde hilo. Kuanzia kulia ni Mkurugenzi Tume ya Umwagiliaji Injinia Seth Lusweme, Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi na Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji Idris Msuya.

Afisa Mkuu toka TANAPA Kanda ya Arusha Vitalis Uruki akiongea na Wanahabari mara baada ya ziara ya kikosi kazi katika bonde la Ihefu katika Wilaya ya Mbalari Mkoani Mbeya.



Na Mwandishi Wetu
KIKOSI cha Kitaifa cha kunusuru Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu, kilichoundwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kilichoko mkoani Mbeya, kimeendelea na ziara yake kwa kutembelea skimu ya Mwendamtitu iliyopo wilayani Mbarali.

Kwa mujibu wa taaifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa vyombo vya habari, katika ziara hiyo, Kikosi kazi kiligundua jinsi ambavyo miundombinu ya skimu hiyo inavyopoteza maji ambayo yalitakiwa kuingia Mto Ruaha.

Aidha, pia kimegundua kuwa skimu hiyo imeanzishwa pasipo kufuata sheria za umwagiliaji kwani haina kibali cha umwagiliaji wala kibali cha matumizi ya maji yanayoingia katika mfereji wa skimu hiyo.

Wakizungumza katika ziara hiyo, wajumbe wamesikitishwa na kitendo cha skimu hiyo cha kutumia maji mengi pasipo kuwa na kibali chochote wala pasipokuwa na miundombinu ya mifereji inayowezesha maji kurudi mto Ruaha Mkuu.

“Katika skimu hii, maji yanatiririka bure na kwa aina hii ya umwagiliaji kamwe mto Ruaha Mkuu hautapata maji, ila tutachukua hatua stahiki,” alisema mjumbe Seth Luswema.

Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali iwasaidie kuwapatia elimu jinsi ya kuendesha skimu hiyo na pia kuelekezwa jinsi ya kuweka miundombinu rafiki kwa ajili ya kuokoa kiasi cha maji kinachopotea. Walisema wao hawana elimu yoyote na hawajui kama wanakosea kwa jinsi wanavyoendesha skimu hiyo.

Kikosi hicho bado kipo mkoani Mbeya wilayani Mbarali kwa ajili ya kuzungukia na kukagua maeneo mbalimbali amabayo yanachangia maji kutokwenda Mto Ruaha Mkuu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment