Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 3 March 2017

ZUIO LA USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA (CONCENTRATES) NA MAWE YENYE MADINI (ORE) KWENDA NJE YA NCHIJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

ZUIO LA USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA (CONCENTRATES) NA MAWE YENYE MADINI (ORE) KWENDA NJE YA NCHI

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuujulisha Umma, Kampuni na watu wanaojihusisha na uvunaji wa madini nchini, kuwa usafirishaji wa makinikia (concentrates) na mawe yeye madini (ore) ya metallic minerals kama vile dhahabu, shaba, nikeli na fedha umesitishwa kuanzia tarehe 02 Machi, 2017. Usitishwaji huu unalenga kuhakikisha kuwa madini yanayochimbwa hapa nchini yanaongezewa thamani kabla ya kusafirishwa kwenda nje hasa kwa ajili ya uyeyushaji (smelting) na usafishaji (refining) ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Aidha, shughuli za uongezaji thamani madini hapa nchini zitatoa fursa ya ajira, mapato na kuhawilisha teknolojia na hivyo kuleta manufaa zaidi kwa Taifa.

Hivyo, ni mategemeo yetu kuwa Kampuni na watu wote wanaovuna madini nchini ambao walikuwa wanasafirisha makinikia ya madini pamoja na mawe yenye madini watazingatia ipasavyo kutosafirisha tena kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uyeyusahji na usafishaji. Wanatakiwa kuanza taratibu za kufanya shughuli hizo hapa nchini. Serikali itatoa ushirikiano unaotakiwa kwa Kampuni au watu watakaojishughulisha na shughuli za uchenjuaji madini hapa nchini hasa uyeyushaji na usafishaji wa madini.

Imetolewa na ;

KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
3 Machi, 2017


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment