Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 12 March 2017

SIR GEORGE KAHAMA AFARIKI DUNIA

 Clement George Kahama enzi za uhai wake.
Na Mroki Mroki
Mwanasiasa mkongwe na waziri wa kwanza wa Ushirika na Masoko Sir George Kahama (89) amefariki dunia hii leo.

Mtoto wa Marehemu aitwae Joseph Kahama amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake Clement George Kahama, al-maarufu Sir. George, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

"Ni Kweli. Mzee wetu amefariki dunia saa 10 jioni hapa Muhimbili," alisema Joseph Kahama kwa ufupi.

Sir George Kahama alizaliwa Novemba 30,1927  na ameacha mke na watoto 11.

Msiba huu ni mzito si tu kwa familia ya Sir George Kahama bali pia kwa taifa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa nchi kabla na baada ya uhuru.

HISTORIA KWA UFUPI.
Sir George Kahama ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa aliye mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika kudai uhuru mnamo miaka ya 1950, hadi kujitawala mwaka 1961, na baada ya uhuru mpaka alipostaafu utumishi wake.

Kahama alijiunga na utumishi wa umma baada ya Mwal Julius Nyerere kupewa fursa na watawala wa kikoloni mwaka 1958, ya kuunda Serikali ya Madaraka wakiwa na lengo la kuhakiki uwezo wa Watanganyika kujiendeshea nchi yao wenyewe.

Wakati inaundwa Serikali ile, ndipo Mwalimu Nyerere alipomwita Sir George kutoka Bukoba, alikokuwa akifanya kazi katika Chama cha Ushirika cha Kahawa (BCU) ili ajiunge na Baraza la Mawaziri la Serikali hiyo, akamteua kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko na mwenyewe (Nyerere) akawa Waziri Mkuu. 

Baadae ilipofika  Desemba 9, 1961, Tanganyika ilitangazwa kuwa huru, na Baraza la Mawaziri lenye madaraka kamili likaundwa, Sir George akiwa waziri wa kwanza wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mbali ya nyadhifa za uwaziri katika wizara mbalimbali, Sir George alipata kuteuliwa kuanzisha taasisi nyeti za kimaendeleo, zikiwa ni pamoja na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Viwanda (NDC); Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA); na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment