Baadhi
ya wakazi wa jiji la Mbeya
wakiwa wamefurika nje ya duka jipya la Vodacom Tanzania katika majengo
ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya wakati wa Uzinduzi wa duka hilo na
kujinunulia simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili
inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania
wakiendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wao walifika katika duka
jipya kupata huduma mbalimblai katika duka jipya la kampuni hiyo
lililozinduliwa jana katika majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya,
Wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart
Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima.
**************
Kutokana
na ongezeko la watumiaji wa huduma ya kifedha wa M-Pesa unaotolewa na
Vodacom Tanzania,Takwimu za TCRA zimeonyesha huduma hiyo inatumiwa
na watu zaidi ya milioni 8,kampuni imejizatiti kusajili wateja zaidi
katika huduma ya ‘Lipa kwa M-Pesa’ sehemu mbalimbali nchini.
Akiongea
na wakazi wa jiji la Mbeya wakati wa Uzinduzi wa duka jipya na
promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba Mkuu wa kanda ya Nyasa
Macfadyne Minja, amesema
kuwa huduma hii ambayo ni salama na inarahisisha maisha ya wananchi
wengi hususani wafanyabiashara inazidi kukubalika ambapo kwa mwaka
jana lengo la kampuni lilikuwa ni kusajili watumiaji 20,000 lakini
wamevuka lengo kwa kusajili watumiaji 40,000 nchini kote.
Alisema
wateja waliochangamkia zaidi ni wale wanaofanya biashara mbalimbali
zinazohusisha kupokea malipo moja kwa moja baadhi zake zikiwa ni
biashara
za maduka ya jumla na rejareja,migahawa,vituo vya kuuza mafuta ya
magari,maduka ya vifaa vya ujenzi.Alisema kutokana na ubora wa huduma
hii biashara za aina mbalimbali zaidi ya 1,000 zimejisajili na zinatumia
kurahisisha mihamala ya malipo ya kibiashara.
“Katika
mkakati wetu wa kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali
huduma hii ya ‘Lipa kwa M-Pesa’ inarahisisha biashara na kuleta usalama
hususani kwa kuwezesha watumiaji kufanya biashara bila kulazimika
kutumia fedha taslimu kama ilivyo katika mataifa mengi
yaliyoendelea,tunatoa wito kwa wafanyabiashara kujiunga nayo na kuwa wa
kisasa na kutoachwa nyuma kiteknolojia”.Alisema Minja
Sitoyo
alibainisha faida nyingine za kutumia huduma hii ni kuwezesha
mfanyabiashara kutuma fedha zake za mauzo kwenye akaunti yake ya M-Pesa
bila
kutozwa gharama zozote,kufanya malipo mbalimbali yanayohusiana na
biashara bila kutozwa gharama za ziada na kuweza kutoa fedha kwa
mawakala wa huduma ya M-Pesa kwa gharama yenye unafuu mkubwa.
“Ni
rahisi sana na nafuu kutumia huduma ya M-Pesa kufanya mihamala ya
malipo kwa kuwa haina gharama zozote za ziada zaidi ya kukatwa thamani
ya bei ya bidhaa anayonunua mteja tofauti na kutoa fedha taslimu kwenye
akaunti ya M-Pesa ambapo kuna makato ,huduma hii pia haichukui muda
kufanya mhamala wa malipo”.Alisema Minja.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu
alisema“Vodacom
inao mtandao mkubwa wa wafanyabiashara ambao tayari wamepatiwa mafunzo
ya kurahisisha biashara zao kwa kutumia huduma ya M-Pesa ambao wako
tayari kumwelekeza mteja anavyoweza
kufaidika kwa kutumia huduma hii hususani kukoa fedha zake za makato ya
kuitumia.Hivi sasa tunatoa ofa maalumu kwa watumiaji wa huduma hii
ambapo kwa kila mhamala anaofanya mteja anapatiwa muda wa bure wa
maongezi ambapo kwa upande wa mfanyabiashara atapatiwa
zawadi kati ya shilingi 2,000/- hadi 100,000/-kwa kila mhamala
kulingana na thamani ya mhamala unaofanyika kwa kuitumia”Alisema Materu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment