Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo vya habari kwa
ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
**************
Na
Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo
vya habari nchini kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Joseph Pombe Magufuli katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini.
Ameyasema
hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo
Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya
kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
“Wanahabari
tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya
kulevya” alisisitiza Mhe. Nnauye.
Ameongeza
kuwa sasa ni wakati wa watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo
katika Wizara yake za Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya
watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.
Aidha
Mhe. Nape amevitaka vyombo vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya
madawa ya kulevya na kuhakikisha haki
inatendeka na vita dhodi ya madawa ya kulevya vinashinda.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment