Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 8 February 2017

RC MJINI MAGHARIBI AKAGUA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA ZANZIBAR


Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipotembelea kujionea maendeleo ya matayarisho ya Tamasha hilo litakalohudhuriwa na Wasanii wapatao 400 kutoka Zanzibar Tanzania na Nje ya Tanzania kwa kutowa burudani ya Sanaa yenye ubunifu kwa kutumia Tamaduni za Kiafrika, akitembelea moja ya Jukwaa la amphitheatre. Likiwa na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni Africa United.  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud akiwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akimtembeza sehemu za kumbi zitakazofanyika kwa Tamasha hilo katika Majengo ya Ngome Kongwe Zanzibar.
Fundi Mkuu wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akitowa maelezo ya kukamilisha kwa ufungaji wa Vyombo vya Muziki na Umeme kwa ajili ya matayarisho ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe 9-2-2017, wiki hii.
Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akitowa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati alipofanya ziara kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamaasha hiyo wakiwa katika Jukwaa kubwa litakalotumika kwa Wasanii kutowa burudani wakati wa maonesho mbalimbali ya Tamasha kwa Wasanii.
Fundi Mkuu wa Tamasha la Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akimuonyesha vyombo vya muziki vitakavyowawezesha Wasanii wakati wakiwa jukwaani wakiimba kujisikia wenyewe sauti zao wakati wa show zikiendelea. 

Mwenyekiti wa Sauti za Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akimuonesha ratiba ya maonesho yote ya Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tamasha hilo katika viwanja vya mambo club ngome kongwe kwa ajili ya matayarisho ya Tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mohamoud akizungumza na wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar alipofika kutembelea kujionea maandalizi ya Tamasha hilo na kuwataka kuitangaza Zanzibar kwa wageni wanaotembelea kujionea maonesho ya Tamasha hilo la Tamaduni za Kiafrika kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka katika Nchi za Afrika.
Wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammrd Mahmoud akitowa nasaha zake kwa wafanyakazi hao wakati alipofika kutembelea maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa Zanzibar tarehe 9-2-2017 
Wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipofika kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamasha hilo kukamilika kwa asilimia mia moja ya maandalizi yake.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.
Imetayarishwa na Zanzinews.com


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment