Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday, 28 July 2017

WANAHABARI WAASWA KUTOANDIKA HABARI ZITAKAZOATHIRI UTALII NCHINI


Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya vyombo vya habari katika sekta ya utalii kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano wa sita ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) mkoani Tanga.
VYOMBO vya habari nchini havipaswi kuandika mambo ambayo yanaweza kuathiri utalii wa Tanzania na badalayake vinapaswa kuwa chachu ya kukuza na kuutangaza utalii. Anaandika Katuma Masamba-Tanga.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas, amesema wanahabari wanapaswa kuhakikisha wanaandika mambo ambayo yataweza kuwavutia watalii kuja nchini na kutembelea vivutio mbalimbali hatua ambayo itasaidia kukuza pato la taifa.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari katika sekta ya utalii kwenye mkutano wa wahariri na wanahabari waandamizi wa kujadili sekta ya utalii nchini unaoendelea jijini Tanga.

"Tunaweza kutumia vyombo vyetu vya habari kuandika vizuri habari za utalii na sekta nzima ya utalii, kwa mfano Kenya huwezi ukakuta wanaandika jambo ambalo wanaona linaweza kuiathiri nchi yao," amesema Dk Abbas.

Waandishi mbalimbali wa habari nchini wakisikilza mada wakati wa mkutano wa Hifadhi za Taifa, Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi nchini unaofanyika jijini Tanga.


VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (wa tatu kutoka kulia) akimweleza jambo Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (wa kwanza kutoka kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana kama Murongo-Kikagati. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano. Wengine pichani ni Maofisa mbalimbali kutoka TANESCO, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Ardhi.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt.  Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda (wa pili kutoka kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa Nsongezi kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya, Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala na Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka TANESCO, Mwesiga Mwesigwa.



Meneja wa Uwekezaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Rwebangi Luteganya (kushoto), akiwaeleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt.  Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano (kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa Nsongezi kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.



Sehemu ya Mto Kagera, unavyoonekana katika eneo la Nsongezi, mpakani mwa Tanzania na Uganda. Maji ya Mto huo yatatumika kuzalisha umeme wa megawati 35 kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wake. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Thursday, 27 July 2017

MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU

 MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde leo amekabidhi mabomba ya kusambazia maji kwa wananchi wa jimbo lake ambao aliwaahidi kufanya hivyo katika harakati za kutatua kero ya maji jimboni kwake.
 Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akikabidhi mambo hayo.
 Wananchi wakimshukuru Mbunge wao.
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, leo amekamilisha ahadi yake katika kijiji cha Matumbulu kwa kutoa mabomba ya kutandazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Km 1 na yenye thamani ya zaidi ya Tshs 8m.

Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo wananchi hao walipigwa na duwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo kubwa la kijiji ilikuwa ni changamoto kubwa na iliyodumu mrefu hali iliyopelekea wananchi kutumia maji ambayo si safi na salama.

Wananchi wengi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine  kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.

Akizungumza katika tukio hilo,  Mavunde amesema"Ni matumaini yangu kwamba ile adha kubwa ya upatikanaji wa  wa maji katika eneo kubwa la kijijini Matumbulu itaisha na kusaidia wanakijiji kupata maji safi na salama kwa wakati"

Aidha Diwani wa kata hiyo,  Emmanuel Chibago amempongeza Mbunge Mavunde kwa anavyojitoa kuwatumikia wanadodoma na kuwaletea maendeleo na hivyo kuwaomba wanadodoma wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi


MAKONDA AGAWA KOPYUTA KATIKA MANIPAA ZA DAR ES SALAAM KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akikabidhi moja ya komopyuta kwa viongozi wa Wilaya na Manspaa za mkoa wa Dar es Salaam ambazo zinalenga kutoa huduma kwa haraka kwa wananchi.
 Watumishi wakichukua Kompyuta hizo hii leo.
KOMPYUTA za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilling Million 170 kwa zimekabidhiwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Manispaa tano za Mkoa huo pamoja na Watu wa Jiji na Mkoa kwaajili ya kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi.

Katika mgawanyo huo kila Manispaa imepatiwa Computer nane huku Ofisi ya Jiji wakipatiwa Computer tano na Ofisi ya Mkoa wakipatiwa Computer tano ikiwa ni ufadhili wa kampun ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono Mheshimiwa Makonda kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri.

Makonda amesema kompyuta hizo zitawekewa Mfumo wa kisasa ujulikanao kama Ardhi E.System utakaoziunganisha idara zote zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi (One stop Center) ili kurahisisha Mwananchi kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi ambapo mwananchi atakuwa na uwezo wa kutuma maombi ya kibali cha ujenzi kwa kutumia simu ya mkononi ke au Computer hata akiwa nyumbani na akapewa majibu yake kwa haraka.

 “Kazi yangu kubwa ni kupunguza mateso,malalamiko na kero za Wananchi dhidi ya kero ya Ardhi, na namna mbili ya kupunguza ni kuwawezesha watendaji kuwa na nyenzo na vifaa vitakavyorahisisha kufanya kazi zao kisasa zaidi kuendana na kasi ya Rais wetu Dr.John Magufuli, namna ya pili ni kusimamia uwajibikaji kwamba kila mmja anatekeleza majukumu yake ili Mwananchi wa Mkoa wa Dar es salaam asipate adha na mateso aliyokuwa akiyapata kwenye Sekta ya Ardhi, umuhimu wa kutoa vibali vya ujenzi ni muhimu katika mji huu unaokuwa kwa kasi barani Afrika” Alisema Makonda.

Aidha kompyuta hizo zitawekewa Mfumo maalumu utakaokuwa ukikusanya Maoni na mapendekezo ya wananchi ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kutuma maoni yao na kero mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta ya Ardhi.

“Tumeishi sana kwenye mfumo wa makaratasi na mafaili, na wakati mwingine kumekuwa na changamoto ya kupotea kwa mafaili na mwananchi kupata adha ya kutoelewa nini afanye maana ataanza upya kutuma maombi, lakini sio hivyo inafanya kazi kuwa ngumu, pia ni chanzo cha rushwa pale mwananchi anapokuwa akisumbuliwa na mtumishi, naamini Compuer hizi zinaenda kukata mzizi wa fitina, Wananchi kulundikana ofisini ni kero kubwa, wananchi kusumbuka kupata huduma ni kero kubwa”, Alisema Makonda.

“Niwaombe watumishi wa Ardhi mtoeni Raisi wenu kimasomaso, mfanyeni ajisikie fahari kufanya kazi na nyie, na namna pekee ya kumpa heshima hii ni kuwatumikia na kuwahudumia vizuri wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwa uaminifu mkubwa na uadilifu, hili linawezekana kwa asilimia mia moja, Aliongeza Makonda.

Hata hivyo ameipongeza Kampuni ya TAMOBA kwa kuamua kunga mkono ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kueleza kuwa Computer hizo zitaenda kufanya kazi iliyokusudiwa ya kupunguza adha kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya TAMOBA Bwana Joseph Kimisha amesema kuwa kampuni yao itaendelea kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Dar es salaam katika masuala mbalimbali ili kuhakikisha wanatatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Katika Makabidhiano hayo pia Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TAMOBA Bwana Otieno Igogo amesema watatoa jumla ya Printer 10 kwaajili ya kusaidia utendaji kwa manispaa za jiji la Dar es salaam ambapo kila manispaa itapata Printer mbili


RAIS MAGUFULI ASIMAMISHWA NA WANANCHI WA TEGETA, AIPONGEZA TCU

 Rais Dkt. John  Magufuli akizungumza na wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, baada ya wananchi hao kusimamisha msafara wake alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
 Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimshangilia Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
 
Rais Magufuli amewasili Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Julai, 2017 akitokea Mkoani Dodoma ambapo akiwa katika eneo la Tegeta Wilaya ya Kinondoni amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake na kuwahakikishia kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na kero na kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

“Kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kusimama hapa Tegeta, nianze kwa kuwashukuru sana, kwa kura nyingi mlizonipa ili niwe Rais wa Awamu ya Tano, nawashukuru CCM, nawashukuru CHADEMA, nawashukuru CUF, nawashukuru ACT na hata wale ambao hawana chama kwani wote kwa umoja wenu mlitanguliza maslahi ya Taifa na kumpa kura mtu ambaye atalisaidia Taifa, na mimi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote na kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu ili Watanzania wote hasa wanyonge ambao siku zote walikuwa wakionewa” amesema  Rais Magufuli

Baadhi ya juhudi alizozitaja kufanyika tangu aingie madarakani ni pamoja na kuondoa ada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, kuongeza mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Shilingi Bilioni 371 hadi kufikia Shilingi Bilioni 483, kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi na kulinda mali za umma hasa madini.

“Kwenye madini tumeibiwa sana, nchi yetu ni kati ya nchi zinazoongoza kwa kuibiwa, tumeibiwa kwa miaka 18, sasa imetosha” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ameipongeza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa kuzuia udahili wa wanafunzi wote wa mwaka kwanza katika vyuo vikuu 19 na kuzuia udahili wa wanafunzi wa kozi 75 katika vyuo vikuu 22 kutokana na dosari zilizobainika wakati wa ukaguzi wa ubora vyuo hivyo uliofanyika Oktoba 2016.

“Ndugu zangu nchi hii ilishakuwa kila kitu hewa hewa, tumegundua wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, kulikuwa na mikopo hewa ya wanafunzi, na naipongeza TCU kwa kufungia baadhi ya vyuo kudahili wanafunzi, nafanya yote haya kwa ajili yenu, nataka tuwe na nchi nzuri” amebainisha Rais Magufuli.


WAZIRI MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA BAINA YA HIFADHI ZA TAIFA, WAHARIRI NA WAANDISHI WAANDAMIZI MKOANI TANGA LEO


Waziri wa Maliasilia na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka baina ya Hifadhi za Taifa, Wahiri na Waandishi wa aandamizi wa habari nchini, ulioanza leo jijini Tanga.Picha zote:Katuma Masamba.
**************
Wanahabari nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia kalamu zao vizuri katika kuandika masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya utalii nchini hatua itakayosaidia kukuza sekta hiyo na patobla taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati akifungua mkutano wa sita wa wahariri na wanahabari waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao umeandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga.

Waziri Maghembe amesema sekta ya habari ina mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini, hivyo wanahabari wanatakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kupitia habari na makala mbalimbali wanazoandika.

"Mchango wa vyombo vya habari ni muhimu sana katika kukuza sekta ya utalii, mmekuwa mnaandika sana lakini naomba muendeleevkuandika zaidi ili tuweze kuwa na sekta ya utalii yenye ustawi mzuri," amesema.

Amesema kwa sasa watu mbalimbali duniani wanafahamu kuhusu vivutio vilivyopo nchini na hiyo ni kutokana na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi amesema wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha watanzania na watu mbalimbali duniani wanavifahamu vizuri vivutio vyvutalii vya Tanzania.

Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hii leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi akizngumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Tanga leo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akizungumza wakati wa mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


RAIS ASISITIZA WASIOENDELEZA VIWANDA MOROGORO WAVIREJESHE SERIKALINI

Rais Dkt John Magufuli Akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa eneo la Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro akitokea Mkoani Dodoma leo Julai 27,2917 na kutoa maagizo kadhaa.


RAIS John Magufuli amewataka watu wote waliobinafsishiwa viwanda mkoani  Morogoro kuvirejesha Serikalini endapo wameshindwa kuviendeleza ili wapewe wawekezaji wanaoweza kuviendeleza na kuzalisha ajira.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo wakati baada ya msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kuelekea Jijini Dar es Salaam kusimamishwa na wananchi wa Morogoro katika eneo la Msamvu mjini humo.

“Ninarudia wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu” amesisitiza ,  Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Manispaa ya Morogoro na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuwaacha wafanyabiashara ndogondogo wa Mji huo waendelee kufanya biashara zao katika eneo la kituo cha mabasi cha Msamvu mjini humo hadi pale utaratibu mzuri utakapowekwa.

Alisema hayo baada ya wananchi wa Morogoro katika eneo la Msamvu kumueleza kero ya kunyanyaswa na Manispaa ambao wamekuwa wakiwafukuza katika maeneo wanayofanyia biashara hasa baada kituo cha mabasi cha Msamvu kujengwa upya.

Magufuli amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro SACP - Ulrich Matei kuhakikisha Askari Mgambo hawawasumbui wafanyabiashara ndogondogo na amewataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewapongeza wakulima wa mazao Mkoani Morogoro kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na amewataja wakulima wa Wilaya ya Kilosa kwa kuongeza uzalishaji kutoka asilimia 42 msimu uliopita hadi kufikia asilimia 82 katika msimu huu.

Kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Morogoro kujitokeza kupata ajira wakati wa ujenzi, lakini amewataka waliojenga katika hifadhi ya reli kuondoa majengo yao kwa hiari.


NAIBU WAZIRI AFYA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA JIMBONI KWAKE



 Muonekano wa ndani wa gari la wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo Wilaya ya Nzega, mkoa wa Tabora.
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,  lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.


 wakishangilia baada ya kukabidhiwa kwa gari hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,  lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega akiongozana na Naibu Waziri Kigwangalla.
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.

Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki. 

Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi  wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa  kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika  ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali za  Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.

Aidha, alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa  kuchangia mafuta ya  ambulance hiyo au gharama yoyote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo. 

“Gari hilo lipatikane kituoni  wakati wote pamoja na dereva. Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu” alieleza Mh. Ngupula.

Ameongeza kuwa gari hilo ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo na kuwa  msaada kwa Tarafa hiyo na wananchi wote watakaopata msaada.

Kwa upande wake, Dk. Kigwangalla amewaomba wananchi waendelee kumuombea kwa kazi anayofanya ikiwemo jukumu la kulitumikia Taifa katika nafasi yake ya Unaibu Uwaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dk. Kigwangalla ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli  kwa kuweza kuwa karibu na Wananchi ikiwemo kushughulikia suala la maji kutoka Ziwa Victoria na kuja Mkoa wa Tabora ikiwemo kuanzia katika Wilaya hiyo ya Nzega na kisha kwenda maeneeo mengine.

“Tunampongeza Rais wetru Dk. Magufuli kwa kuwa karibu na wananchi wake. Tulikuwa nae Mkoani kwetu hapa Tabora na amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara na ule wa maji safi yatakayotoka Ziwa Vitoria. Shida ya maji kwa wananchi wa Nzega inaenda kuwa histoa kwani Maji hayo yatakuja hapa na kisha kwenda maeneo mengine. Rais wetu anatupenda na tuendelee kumuunga mkono hasa juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi yetu na pia katika kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi wa Taifa letu

Mimi Mbunge wenu pia muendelee kuniombea na kila siku mawazo yangu na akili yangu ipo pamoja nanyi ndio maana nimeweza kuwaletea gari hili la wagonjwa, na pia kufanikisha kuandaa kambi maalum ya matibabu bure ya wiki moja kwa wananchi wote wa Nzega bure” alieleza Dk. Kigwangalla.

Tukio hilo la ukabidhi wa gari hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Jimbo hilo na wale wa jimbo jirani ikiwemo Bukuene, Viongozi wa ulinzi na Usalama pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nzega.