Na. Mwandishi Wetu, MAELEZO
Serikali
kupitia Kampuni Hodhi ya Reli (RAHCO) imetangaza mchakato wa awali wa zabuni ya
ununuzi wa vichwa na mabehewa kwa ajili ya treni ya umeme itakayotumika katika
reli ya kisasa (Standard Gauge) ambayo ujenzi wake unaendelea.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa ameithibitishia Idara ya Habari
(MAELEZO) kuanza kwa mchakato huo ambao unafuata taratibu za kimataifa za ununuzi
kwa njia ya ushindani.
Kwa
mujibu wa tangazo la zabuni, jumla ya vichwa 14 vya treni ya umeme kwa ajili ya
kusafirisha mizigo na vichwa viwili vya treni ya mizigo inayotumia mafuta
vinahitajika.
Aidha,
RAHCO pia imetoa zabuni ya ununuzi wa vichwa vitano vya treni ya abiria ya
kisasa inayotumia umeme (Electric Multiple Units) ambapo kila kimoja kitakuwa
na uwezo wa kuvuta mabehewa 60 yenye kuchukua abiria 1,800.
Katika
mabehewa hayo ya abiria, mabehewa 15 yatakuwa ni ya kiwango cha daraja la
kwanza na mengine 45 ni daraja la pili.
Mbali
na mabehewa ya abiria, zabuni hiyo inajumuisha ununuzi wa mabehewa mengine
zaidi ya 1,500 yenye muundo tofauti kwa ajili ya kubebea aina mbalimbali za
mizigo.
Pamoja
na sifa mbalimbali zilizo ainishwa katika tangazo la zabuni, moja ya sifa za
reli hiyo ya kisasa ni kuhimili treni ya abiria yenye uwezo wa mwendo kasi wa
kilometa 160 na mabaehewa yenye juma ya urefu wa mita 2000, wakati ile ya
mizigo yenye uwezo wa kwenda kasi ya kilometa 120 kwa saa.
Kwa
mujibu wa tangazo la zabuni, mwisho wa kuwasilisha nyaraka za zabuni ni Januari
30, mwaka huu.
Tayari
awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hii kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro
inaendelea na wakati huo huo tayari Serikali imesaini mkataba kwa ajili ya
awamu ya pili ya ujenzi kutoka Morogoro hadi Makutupola mkoani Dodoma.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment