Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 3 October 2017

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA ALAT - DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiongea machache wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw. Gulma Hafeez Muccadam akisoma risala yao mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mhe Kassim majaliwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ya kumbukumbu na wadau wa maendeleo na wafadhili wakuu wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita Baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya Kigogo wakati akiwasili kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea banda la benki ya NMB na mabanda mengine kabla ya kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU. 
*******************

RAIS  Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa mamlaka za Serikali za Mitaa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinafanywa kutetea rasilimali za taifa, kujenga uchumi na kurekebisha dosari zinazosababisha kero kwa wananchi ili kujenga Tanzania mpya. 

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kujumuisha viongozi na watendaji wakuu wa Majiji, Manispaa, Miji na halmashauri za Wilaya.

Rais Magufuli ametaja juhudi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani miezi 23 iliyopita kuwa ni pamoja na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali kutoka Shilingi Bilioni 850 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.3, kuongeza bajeti ya maendeleo kutoka asilimia 26 hadi kufikia asilimia 40, kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo kwa kutoka ruzuku ya Shilingi Bilioni 23.868 kila mwezi, kuongeza bajeti katika huduma za afya na kutekeleza miradi ya maji katika miji na vijiji mbalimbali nchini.

Juhudi nyingine ni kuimarisha miundombinu ya usafiri kwa kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya Dar es Salaam na Morogoro na baadaye Morogoro – Dodoma kwa Shilingi Trilioni 7, kununua ndege 6 kwa ajili ya shirika la ndege la taifa, upanuzi wa bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, Ununuzi wa meli mbili za ziwa Nyasa, ujenzi wa viwanja vya ndege, barabara za juu Jijini Dar es Salaam na barabara ya njia 6 ya Dar es Salaam – Chalinze pamoja na kuendeleza mradi wa mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam (BRT).

Rais Magufuli ameongeza kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawatts 1,460 zinazolishwa hivi sasa hadi kufikia megawatts 5,000 ifikapo mwaka 2020 kwa kujenga miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi na kujenga mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge), kuongeza vijiji 7,873 vitakavyopata umeme na hivyo kufikia vijiji zaidi ya 12,259 ifikapo mwaka 2021, kusimamia biashara ya madini kwa manufaa ya Watanzania, kusimamia ipasavyo usambazaji wa pembejeo na kujenga mazingira bora ya uwekezaji.

Rais Magufuli amewahakikishia viongozi hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kufanya juhudi kubwa zaidi zenye manufaa kwa nchi na hivyo ametoa wito kwa viongozi hao kutoa ufafanuzi wa dhamira hiyo kwa wananchi na kushirikiana kutekeleza mipango na miradi kwa kutanguliza maslahi ya taifa.

“Nataka niwaambie ndugu zangu adui yetu sio vyama vya siasa, adui yetu ni wanaotuibia rasilimali zetu, hivyo twende pamoja, tushirikiane kuijenga nchi yetu” amesisitiza Rais Magufuli na kuwataka viongozi hao kuondoa tofauti na migogoro iliyopo kwenye mamlaka zao.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa kazi kubwa wanayoifanya  kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali na mipango ya Serikali na amewahakikishia kuwa changamoto zinazowakabiri zitafanyiwa kazi ili kuongeza ufanisi wa mamlaka hizo.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja wadau mbalimbali wa maendeleo wa halmashauri kutoka taasisi na mataifa mbalimbali.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment