Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 8 July 2017

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA KINYEREZI ll

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Mdoe, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Mdoe, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya maendeleo ya mradi kutoka kwa Meneja mradi Stephen Manda, wakati akikagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Tito Esau, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiongea na Wananchi wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. BOFYA HAPA

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco Balozi Dkt. James Nzagi, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.
*******************
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameelezwa kuridhishwa na hatua za ujenzi wa mradi wa umeme wa Kinyerezi II, huku akiwataka wakandarasi na watumishi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati. Anaandika Katuma Masamba.
 
Aidha, Waziri Majaliwa amesifu utendaji kazi wa wakandarasi na wafanyakazi wengine, ambao umefanikisha ujenzi wa mradi huo kufikia asilimia 66.

Waziri Majaliwa ameelezwa kuridhishwa kwake baada ya kukagua mradi huo leo (Jumamosi) ambapo ameawataka wakandarasi hao na wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

"Mkakati wa serikali ni kuongeza kiwango cha umeme nchini, tunataka kuongeza umeme ili ufike hadi vijijini. Kikubwa niwasihi mfanye kazi ili hadi kufikia mwezi wa nane mwaka ujao uwe umekamilika kwa asilimia 100," amesema.

"Lakini pia nimeambiwa kuwa mradi huu utakapokamilika utakuwa na teknolojia ya kisasa na kwa Afrika Mashariki na Kati sisi ndio tutakuwa wa kwanza, teknolojia ambayo tunaweza kutumia joto kuzalisha umeme, hivyo tutumie teknolojia hiyo kuzalisha umeme mwingi,".


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment