Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 11 July 2017

TSN YAPONGEZWA KWA UMAKINI

 SHEHE wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum (kulia) akiwa katika banda la Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
SHEHE wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ameipongeza Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kuzalisha bidhaa zilizo makini, jambo linaloonesha jinsi ambavyo serikali inafanya kazi nzuri. Anaandika Lucy Lyatuu.

Kampuni hiyo ni wazalishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo, Sunday News, HabariLeo Jumapili na SpotiLeo pamoja na majarida mbalimbali.

Shehe Salum alisema hayo jana wakati akiwa katika banda la kampuni hiyo lililoko katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa.

Alisema magazeti hayo yameboreshwa kwa kiwango kikubwa na yamekuwa yakitoa taarifa sahihi katika jamii na hata juu ya utendaji mbalimbali wa serikali.

Aliwasihi waandishi hao kuendelea kuzingatia maadili, tija na ufanisi katika kazi zao ili kwamba Watanzania waendelee kuwaamini kwani wengi wao wameamka, wanaelewa na ni wasomaji wakubwa wa magazeti.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment