Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 6 July 2017

RAIS MAGUFULI AMTHIBITISHA KAZINI BOSI WA TTCL

RAIS John Magufuli amemteua, Waziri Waziri Kindamba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo imeeleza kuwa Uteuzi wa Kindamba umeanza Julai 4, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Kindamba alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu alipoteuliwa na Rais Dk Magufuli Septemba 23, 2016 akichukua nafasi ya Afisa Mtendaji wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura.
 
ELIMU NA SIFA ZA WAZIRI WAZIRI KINDAMBA
Kindamba alipata elimu katika Chuo Kikuu cha Sunderland – Uingereza, alipotunukiwa Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA), kabla ya hapo alipata elimu katika Chuo Kikuu cha London Metropolitan – Uingereza, Shahada ya BA (Hons), Benki, Uchumi na Sheria (Daraja la kwanza)

Aidha pia aliwahi kupata elimu katika Chuo Kikuu cha Leicester- Uingereza, Stashahada ya Stadi za Utawala (Benki na Huduma za Fedha).

Kindamba alisoma masomo ya sekondari katika shule za Sekondari za Tambaza, na Azania, Dar es Salaam.
Katika uzoefu wa kazi, Kindamba, alipata kufanya kazi Diamond Trust Bank (T) Ltd. akiwa ni Meneja wa Tawi na Mjumbe wa Timu ya Viongozi Waandamizi , Tawi la Morocco,  tangu mwaka 2011 hadi alipoteuliwa kujiunga na TTCL.

Pia aliwahi kufanya kazi katika Benki ya NBC.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment