Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi
wengine akifungua mradi mkubwa wa maji
katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia
wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo
ya mradi huo mkubwa wa maji kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na
Usafi wa Mazingira Antony Sanga wakati alipoanza ukaguzi wa mradi huo kabla ya
kuufungua.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya
kufungua mradi huo wa maji Wilayani Sengerema.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia
wanafunzi wa Sekondari mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema vijijini
wakati akielekea kuzindua mradi wa Maji.
**********************
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli, leo Julai 4, 2017 amehitimisha
ziara yake ya kikazi ya Siku Mbili Mkoani Mwanza kwa kuzindua mradi wa Uboreshaji wa huduma ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema.
Mradi huo wa maji umetekelezwa
chini ya mpango wa maji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya
shilingi bilioni 22.4. Mradi wa Maji Safi mjini Sengerema ulioanza tangu mwaka
2011 unatarajiwa kuwahudumia wakazi 138,000 ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa Mradi huo, Rais Dkt. Magufuli amesema kukamilika kwa
mradi huo kutamaliza tatizo la maji la muda mrefu kwa wakazi wa Sengerema na
maeneo ya jirani.
Rais Dkt.
Magufuli amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kuutunza na kuhakikisha
hawaharibu vyanzo vya maji katika eneo hilo la ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na
kuacha uvuvi haramu ambao umekuwa na madhara makubwa kwa wananchi.
Aidha, ameuagiza
uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Vyombo vya Dola kuchukua hatua kali dhidi ya watu
wanaochafua vyanzo vya maji katika eneo la Ziwa Victoria.
Katika hafla hiyo
ya Uzinduzi wa mradi wa maji Kada wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA HamisiHussein Maarufu TABASAM,
ameamua kuachana na chama chake na kujiunga na CCCM.
Rais Dkt.
Magufuli ameendelea kusisitiza msimamo wa Serikali kuwa hakuna mwanafunzi
atakayepata ujauzito ataruhusiwa kuendelea na masomo na ameyataka Mashrika
yasiyo ya Kiserikali ambayo yamekuwa yakipinga uamuzi huo kufungua Shule zao
wenyewe ambazo zitawasomesha wanafunzi wanaopata ujauzito.
''Haiwezekani
Serikali itoe pesa kuwasomesha wanafunzi halafu wapate mimba waendelee na
masomo hilo haiwezekani, hizo NGOs zinazotetea hali hiyo zikitaka zijenge shule
kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi watakaopata ujauzito''amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli
amezungumzia uamuzi wa Serikali kupeleka Miswada Mitatu ya dharura Bungeni kuwa
unatokana na umuhimu wa hilo katika kutetea maslahi mapana ya nchi na
kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi.
Rais Magufuli
amewaonya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wenye nia ya kugombea nafasi
mbalimbali katika Uchaguzi wa Chama hicho kutojihusisha na rushwa kwa vile
rushwa ni adui wa haki, hivyo, atakayebainika kutumia rushwa atapoteza sifa ya
kuwa Mgombea.
Akizungunzia
ujenzi wa barabara ya kutoka Kamanga hadi Sengerama kwa kiwango cha lami, Rais Dkt. Magufuli amesema kwa sasa
Serikali imeshampata mkandarasi kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na
usanifu ili barabara hiyo ianze kujengwa katika kutimiza ahadi aliyoitoa wakati
wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Rais Magufuli pia
amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchni kufafanua kwa wananchi na kusimamia
uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo zaidi ya 80 katika mazazo ya Kilimo, tozo 7
za Mifugo na tozo 5 za Uvuvi ambao lengo lake ni kuwaondolea kero wananchi.
Aidha, amesema
Serikali inafanya uchambuzi ili kubaini wale wote waliotoa pembejeo hewa na
atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya
Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji na halikadhalika
leseni ambazo zimeisha muda wake. Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na
wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati
akiwa njiani kuelekea Chato.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment