Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 8 July 2017

MBUNGE VITI MAALUM CCM ANUSURIKA KIFO AJALINI LEO



 Toyota VX lenye namba za usajili T329 DGK alilokuwa akisafiria Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Ruvuma, Sikudhani Chikambo (picha ndogo) iliyopata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja leo mchana eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
MBUNGE wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma CCM, Sikudhani Chikambo amenusurika kifo katika ajali ya barabarani hii leo Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Anaandika John Nditi-Morogoro.

Mbunge huyo pamoja na watu wengine watano walikuwa wakisafiri kutoka Dodomna kwenda jijini Dar es Salaam ndipo gari walilokuwa wakisafiria Toyota VX lenye namba za usajili T329 DGK,  kupasuka gurudumu na kuacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha ndugu wa Mbunge huyo.

 Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alikolazwa kwa matibabu alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wake kuwepa shimo lakini kutokana na ukubwa wa shimo hilo gurudumu lilitumbukia na kupasuka kisha gari kupoteza muelekeo na kupinduka mara tano.

“Dereva alikuwa anakwepa shimo, lakini kutokana na ukubwa wa shimo tairi lika tumbukia na kupasuka gari iliyumba na kupoteza mwelekeo …na kupinduka mara tano kabla ya kusimama,”alisema Sikudhani.

Alisema aliyepoteza maisha ni ndugu wa karibu wa kiume aliyekuwa akiishi Dodoma na kufanyia kazi za ujenzi wa nyumba.

Alisema baada ya ajali walikimbizwa Hospitali ya Kanisa Katoliki Dumila na baadae  kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro.

Wabunge Mbalimbali wa mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Mbunge wa Viti  Maalumu Vyuo Vikuu, Dk Jasmine Tisekwa walimtembelea na kumjulia hali.

Dk Tisekwa ndiye alimsaidia Mbunge mwenzake na majeruhi kuletwa hostitali kuu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment