Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 11 July 2017

MAKINDA AISHAURI SERIKALI KUAGIZA WANAFUNZI WA BWENI WOTE NCHINI WAWE NA BIMA YA AFYA

 Spika Mstaafu wa Bunge na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF), Anne Makinda akimkabidhi kadi ya Bima ya Afya ya Toto Kadi mmoja wa watoto aliyekatika huduma hiyo na wazazi wake.
 Spika Mstaafu wa Bunge na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF), Anne Makinda (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wanachama wa NHIF, Elentruda Mbogoro, wakati Mwenyekiti huyo alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayofanyika viwanja vya Mwl. Julis K Nyerere, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda ameiomba serikali kutoa agizo kwa wanafunzi wanaokwenda shule za bweni kuwa na bima ya afya, ili kupunguza gharama kwa wazazi pindi wanapougua wakiwa masomoni. Anaandika Katuma Masamba.


Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu ametoa ombi hilo katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa (DITF) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius K Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.


Amesema licha ya wazazi kutakiwa kulipia gharama za matibabu kwa mtoto wake wakati anapojiunga na shule, lakini mtoto huyo anapoumwa akiwa masomo hulazimika kurudishwa nyumbani ambapo mzazi huingia gharama za matibabu.


"Shule zote zinapokuwa zimechagua wanafunzi wa kujiunga na shule zao huwa zina maelekezo, ikiwa in pamoja na kila mzazi kuchangia matibabu ya mtoto wake shuleni".


"Serikali ingetoa amri katika suala la bima ya afya kwa kila mwanafunzi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma. Unajua inauma sana mzazi unalipa hela ya matibabu lakini mtoto akiumwa unapigiwa simu umfate," amesema Makinda.


Amesema kama serikali itatoa amri ya wanafunzi kuwa na bima ya afya itawawezesha wazazi kuwa na uhakika wa afya za watoto aao hata kama wataugua wakiwa safarini watapata huduma za matibabu katika vituo vya afya na hospitali mbalimbali nchini.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment