Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 24 July 2017

KONGAMANO KUBWA LA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA UTURUKI KUFANYIKA HIVI KARIBUNI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akizingumza katika kamkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana uliolenga kuufahamisha umma juu ya kongamano la kibiashara litakalofanyika Julai 27,mwaka huu baina ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Ofisa anaeshughulika na masuala ya Biashara kutoka Ubalozi wa Uturuki nchini, Onur Tekyildiz. 
 *****************
TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Chama cha Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) pamoja na Jumuia ya wauzaji nje ya nchi ya Uturuki wameandaa kongamanonla kibiashara baina ya kampuni za Uturuki na Tanzania inayotaraji kufanyika Julai 27,mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia Kongamano hilo Mkurugenzi Mtendajinwa TPSF, Godfrey Simbeye amesema lengo kuu la Kongamano hilo la kibiashara ninkuongeza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya nchi hizo mbili pamoja na kubadilishana ujuzi na utaalam katika masuala ya kibiashara.

Simbeye alisema zaidi yanwashiriki 200 wanataraji kushiriki, huku akitoa wito kwa watanzania kutoka sekta mbalimbali hasa za ujenzi, kilimo na viwanda vya nguo kujitokeza na kujiandikisha kwaajilinya ushiriki wao.

"Hakuna adda ya ushiriki katika kongamano hilo, na nafasi ni chache maana tunataraji tuwe na washiriki takriban 200 ambao watakuja kukutana na makampunibya uturuki na kubadilishana uzoefu, hivyo tunatoa rai walio na nia ya kushiriki kujiandikisha mapema,"alisema Simbeye.

Aidha alisema kongamanobhilo litalenga zaidi katika sekta za umeme na vifaa vyake, mashine za kilimo, bidhaa zitokanazo na chuma, nguo na ushonaji, kemikali, vifaa vya magari na vipuri, saruji, ujenzi, Mahospitali, mazao ya vyakula na malighafi nyinginezo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment