Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 17 June 2017

MANGULA AWAONYA MAKATIBU WASALITI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amesema chama hicho hakitawavumilia Makatibu wa chama hicho kuanzia ngazi ya Mashina hadi Taifa wanaoendelea kukisaliti chama hichokwa kupanga safu za wagombea.

Amesema hawatasita kuwavua uanachama makatibu watakaobanika kufanya usaliti na kupanga safu za wagombea katika chaguzi ndogo zinazoendelea ndani ya chama hicho.

"Bado kuna baadhi ya makatibu wa ngazi ya shina hadi taifa wanaendelea kupanga safu katika chaguzi zinazoendelea, hawa tutawashughulikia,"  amesena Mangula wakati akizungumza kwenye mkutaano wa kupokea tamko la kumuunga mkono Rais John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho kwa utendaji kazi wake ikiwemo kuzuia mchanga wa madini "Mashobo" kusafirishwa nje ya nchi.

Amesema makatibu watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa kanuni za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufukuzwa ndani ya chama


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment