Mgeni Rasmi, Naibu wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye oia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Angelina Mabula akizungumza kabla ya kutunuku vyeti kwa wahitimu.
Naibu wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye oia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Angelina Mabula, akitunuku vyeti kwa wahitimu.
Naibu wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye oia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Angelina Mabula, akitunuku vyeti kwa wahitimu.
Wahitimu wa mafunzo katika picha na mgeni rasmi.
Na Alexander Sanga,Ilemela
Naibu waziri wa Ardhi,nyumba na makazi Angelina Mabula amewasisitiza vijana wajitaidi kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa kuanzisha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali ili waweze kujiajiri.
Akizungumza katika kuhitimisha mafunzo ya muda mfupi ya utengenezaji viatu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar-es-salaam (DIT),Kampasi ya Mwanza,Mabula alisema wahitimu hao wanatakiwa kujituma sana ili waweze kufanya kazi kwa bidii.
Mabula ambae pia ni Mbunge wa wilaya ya Ilemela alipongeza chuo hicho kwa kuendlea kutoa mafunzo mbali mbali kwa vijana ikiwa kama njia mmoja wapo ya kupunguza tatizo la ukosefu wa ujuzi wa vijana.
Mabula aliwaomba wahitimu hao watumie mafunzo waliopata katika kutengeneza vikundi mbali mbali vya ujasiriamali katika kuhakikisha wanatimiza lengo la kutengeneza nchi ya viwanda.
Naibu Waziri aliwaagiza wanafunzi hao wahakikishe viatu wanavyotengeneza wanapeleka katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba na NaneNane ili waweze kupata Soko la bidhaa hizo.
Mafunzo hayo ya muda mfupi ya utengenezaji wa viatu yalikuwa ni ya miezi miwili ambayo yalikutanisha wanafunzi mbali mbali kutoka mikoa tofauti.
Mkuu wa chuo hicho,Dr Albert Mmari alisema mafunzo hayo yatasaidia vijana kuepuka na tatizo la ukosefu wa ajira endapo wakitumia ipasavyo taaluma walioipata.Dr Mmari aliwaagizia wahitimu kuhakikisha wanatumia ngozi iliobora katika kutengeneza viatu.
Mmari aliomba serikali ijitaidi kuleta wanafunzi mbali mbali chuoni hapa katika kuhakikisha wanapata elimu tofauti za ufundi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, John Wanga ameiomba serikali kuboresha mashini zinazotumika chuoni hapo kwakuwa nyingi ni za tokea 1980.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment