Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 2 March 2017

RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA YA SIKU NNE MIKOA YA PWANI,LINDI NA MTWARA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt.  John Pombe Magufuli, leo  Machi 02, 2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Leo asubuhi Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani na baadaye ataelekea Mkoani Lindi.

Kesho Machi 03, 2017 Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Lindi na keshokutwa  Machi 04, 2017 atafanya ziara yake Mkoani Mtwara.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment