Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 9 March 2017

KATIBU MKUU UN AIMWAGIA SIFA TANZANIA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga wakati Katibu Mkuu huyo aliposimama kwa muda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Bi. Mindi Kasiga naye akiagana na Mhe. Guterres
Mhe. Guterres akiagana na Dkt. Mahiga mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo yao.
***************
Na Mroki Mroki
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameisifu Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake za kutafuta amani nchini Burundi.

 Guterres alitoa pongezi hizo wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa jijini Dar es Salaam akitokea nchini Kenya.

 Katibu Mkuu huyo mpya wa UN alisimama kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga.

 Pamoja na mambo mengine Guterres alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa serikali kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

  “Tanzania imekuwa kinara wa amani Afrika na duniani na naipongeza kwa dhati katika jitihada zake inazozifanya za kutafuta amani ya Burundi na katika nchi nyinge za ukanda huu,” alisema Guterres.

 Aidha alisema anatambua mzigo mkubwa inaoupata kama nchi  kutokana na kuendelea kupokea wakimbizi kutoka nchini Burundi, na kuahidi UN kuendelea kuunga mkono jitihada za kutafuta suluhu ya kisiasa nchini humo.

 Kwa upande wake;  Balozi Mahiga aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais John Magufuli kuhusiana na hatua iliyofikiwa ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi na ushiriki wa Tanzania katika vikosi vya Umoja wa Mataifa vya ulinzi wa amani Mashariki wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

 Balozi Mahiga pia alisema kama nchi wamefurahishwa na ujio wake na Rais amempa mwaliko rasmi wa kufanya ziara nchini.

 Aidha alimweleza kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano wao ujao wana mpango wa kuwasilisha hoja maalum kuhusu hali ya kisiasa nchini DRC.

 Mbali na kufanya ziara nchini Kenya, Katibu Mkuu huyo wa UN alitembelea nchi ya Somalia na kukutana na Rais mpya wa nchi hiyo, Mohamed Abdullahi Mohamed, ambapo aliagiza Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua kuepusha balaa la njaa nchini Somalia, kutokana na  hali mbaya ya ukame.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment