Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday, 4 August 2017

NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIKALI


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  Jenista Mhagama (kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia Mashine za BVR. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Uchaguzi,  Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA wa Tume,  Mwamvita Solo.
 


RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AWASILI TANGA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN MAGUFULI

Rais wa Uganda, Yoweri Museven akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Tanga jana tayari kuhudhuria sherehe za uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga. Marais John Magufuli na Rais Museven watashiriki katika uwekaji huo wa jiwe la msingi. (Picha na Mroki Mroki).
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika kesho katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Tanga kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Tanga.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake wakati akielekea kwenye Dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ya Tanga.


Thursday, 3 August 2017

RC SHIGELA WA TANGA ALEZEA FURSA ZITOKANAZO NA BOMBA LA MAFUTA LA HOIMA-TANGA


Wednesday, 2 August 2017

RC MAKONDA APOKEA MSAADA WA KOMPYUTA 100 KUTOKA NIDA TEXTILE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amepokea Jumla ya Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.

Makonda amesema Computer hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi  20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.

Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.
Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza  uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.

Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi  viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda atapata atajua.

Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari na mhalifu ambae matukio matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.

“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.

Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Dar es Salaam.


DAWASCO YASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA UWAZI

Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA KAJUNASON BLOG/MMG.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco).
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa na watendaji wengine wakati wakiimba wimbo wa 'Tanzani', 'Tanzania'.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema ameapa kuwashughulikia watumishi wachache chini ya wizara yake ambao bado wanaendekeza maisha ya ujanja ujanja kazini. Profesa Kitila ameitoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) kwenye ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. 

 Amesema ingawa Dawasco imefanikiwa kuboresha huduma zake, lakini wapo watumishi wa chache ambao bado wanafanya kazi kwa ubabaishaji. Amesisitiza kuwa zama za ujanjaujanja zimekwisha na wale wachache wanaoshiriki mbinu za kulihujumu shirika hilo hawatavumiliwa na watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa watakaobainika. Wakati huo mhuo, Profesa Mkumbo amewashukuru watendaji na watumishi wa Dawasco akibainisha kuwa siku hizi simu za malalamiko anazopigiwa na wateja kuhusu huduma za maji zinazotolewa na Shirika hilo zimepungua sana. 

Amesema hali hiyo inatokana na Dawasco kuboresha huduma zake. Amesema hivi sasa anatumiwa ujumbe mfupi wa kupongezwa kuhusu huduma za zinatolewa na Dawasco na kulitaka shirika hilo kuendelea kuchapa kazi ya kutoa ya kuwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. “Hongereni kwa huduma nzuri mnazitoa kwa wakazi wa mikoa hii. Nyie ndiyo taswira ya Serikali katika utoaji wa huduma za maji. 

Bila nyie Ukatibu wa Mkuu hauna maana kwa mkoa wa Dar es Salaam hata waziri na wizara kwa ujumla,” amesema Profesa Mkumbo. Profesa Mkumbo amesema wizara yake haina mipaka katika utendaji kazi na kwamba ipo wazi kuwasiliana mtendaji yeyote atakayetaka huduma.


UWEKEZAJI ZAIDI WAHITAJIKA KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA

Mkuu wa Utawala na Maendeleo ya Uwezeshaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
PAMOJA na serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, ikiwa ni asilimia 17 ya bajeti nzima, mazingira ya kufundisha na kufundishwa nchini bado si mazuri. Akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam pamoja na kuwekwa maeneo ya kuangaliwa kwanza ipo haja ya kufanya zaidi ili kufikia malengo. Dk Katabaro katika mada yake alisema kwamba pamoja na serikali kutenga zaidi ya TZS 1.366,685,241,000.00 katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi huku Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) ikipatiwa sh 201,655,446,000/- kwa ajili ya elimu, alisema kwamba anaona ipo haja ya kuongeza nguvu katika maeneo kadhaa ili kuweka sawa mazingira ya kufundisha na kufundishwa.
 Katika mjadala huo wa kitaifa uliodhaminiwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Katabaro alisema kwamba kwa sasa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinakosekana katika shule nyingi na taasisi zinazohusiana na elimu na hivyo kukwamisha ufanisi na tija katika elimu. Aidha katika mada yake alitaka juhudi inayofanywa ya kuweka sawa mizania ya walimu pale walipo wengi kuhamishwa inabidi iendelee ili kuweka uwiano sawa wa elimu nchini. Pia alisema kuwa uwiano wa sasa wa walimu nchini sio sawa huku katika masomo, baadhi yakiwa na walimu wa ziada na mengine yakiwa na upungufu mkubwa. Profesa wa Menejimenti ya Elimu kutoka Skuli ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Eustella Bhalalusesa (katikati) akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha muwasilisha mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption] Mwaka 2016 kwa mujibu wake kulikuwa na walimu wa ziada katika masomo kadha huku kukiwa na upungufu katika masomo mengine hasa Hesabu na Sayansi: Basic Mathematics – 7,291 (Upungufu);Biolojia – 5181 (Upungufu);Kemia – 5373 (Upungufu);Fizikia – 6873 (Upungufu);Kilimo 508 (Upungufu);Kingereza– 1267 (ziada); Jiografia – 3281 (ziada); Historia – 4764 (ziada) na Kiswahili – 4795 (ziada). Pamoja na masomo Dk. Katabaro aliangalia bajeti hiyo katika maeneo muhimu yanayofanya mtoto kuwa na akili kama viwanja vya michezo na upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya kunywa na usafi. Maji haya ni muhimu sana kwa watoto wa kike ambao usafi wao ndio siri ya mahudhurio ya shule kila siku. Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption] Mada hiyo pia ilitahadharisha kuhusu takwimu ikitaka zitumike vyema ili kuondoa mipango mibovu hasa ya uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza na wale wanaoingia kidato cha kwanza. Wakati huo huo katika mada iliyowakilishwa kwa pamoja kati ya Profesa haidari Amani na John Shilinde, kilimo pamoja na kutegemewa na wengi na kuwa chachu ya maendeleo ya viwanda bajeti yake iliyotengwa bado ni ndogo Walisema kwamba sekta hiyo ilipata kiasi cha karibu asilimia 10 ya bajeti nzima, bajeti ambayo ukiiangalia utaona kwamba haiwezi kubadili kilimo. Wamesema kwamba kilimo ambacho huajiri asilimia 70 ya wananchi ikichangia asilimia 28 ya pato la taifa huku ikipatia asilimia 30 ya mapato ya kigeni na kuchangia asilimia 65 ya mali ghafi, bado sekta haijapewa nguvu za kutosha kusonga mbele. Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo, Peter Lanya akizungumza machache kabla ya kumkaribisha muwasilishaji mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption] Wamesema kilimo kitabadilika kwa fedha za utafiti na sayansi na ubunifu ili kuiweka sekta katika hali bora zaidi. Walisema kwamba sayansi na ubunifu ni kichocheo kikubwa cha mabadiliko katika kilimo. Wataalamu hao walitaka bajeti zaidi kwa ajili ya utafiti na maendeleo, kilimo cha umwagiliaji, kuongeza ruzuku, kuboresha kilimo cha kisasa cha kutumia zana kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza kazi zenye staha vijijijni, kuongeza mnyororo wa thamani na matumizi endelevu ya ardhi na maji. Mtafiti Mshiriki Mwandamizi kutoka ESRF, John Shilinde akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Hildegalda Mushi kutoka COSTECH akichangia maoni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mshiriki William Mhoja akichangia mada kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof Honest Prosper Ngowi akishiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.