Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 11 March 2018

MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) amemsimamisha kazi Bwana Emmanuel Barabara, Mhifadhi Wanyamapori Mkuu ambaye pia ni Mkuu wa Kanda – Pori la Akiba Rukwa, lililopo wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi, kuanzia jana tarehe 10 Machi, 2018 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

 
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dr. Aloyce K. Nzuki imesema Dk. Kigwangalla amechukua uamuzi huo kufuatia taarifa za raia wema kuwa Bwana Barabara amekuwa akishirikiana na majangili katika kuhujumu rasilimali za misitu nchini.
 
Aidha, Waziri Kigwangalla ameagiza iundwe Kamati ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo, na endapo mtuhumiwa huyo atakutwa na hatia, hatua kali za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma ili iwe fundisho kwa wengine.

Tunatoa onyo kali kwa watumishi wa Wizara wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa rasilimali za Misitu, Wanyamapori na Malikale kuacha mara moja kwani hatutosita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo ikiwemo kufukuzwa kazi.

Watumishi wote wa Wizara wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya uhifadhi wa rasilimali za nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment