Meneja Mauzo Samsung, Lailatu Jethwa (kushoto)
akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni yao mpya ya ‘Nunua sajili
na Ushinde’ inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni,
Meneja wa Samsung Nchini,Rayton Kwembe na Meneja bidhaa za majumbani wa
Samsung,Elias Mushi .
Meneja Mauzo Samsung, Lailatu Jethwa (kushoto) akiwaonyesha
waandishi wa habari bidhaa zinazohusishwa katika kampeni yao mpya ya
‘Nunua sajili na Ushinde’ inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati
ni Meneja wa Samsung Nchini Rayton Kwembe, akifatiwa na meneja
bidhaa wa Samsung, Elias Mushi na Meneja wa Phyramid Consumers
Meneja Mauzo Samsung, Lailatu Jethwa (kushoto) akiwaonyesha
waandishi wa habari bidhaa zinazohusishwa katika kampeni yao mpya ya
‘Nunua sajili na Ushinde’ inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja wa Samsung Nchini Rayton Kwembe. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
*************
SAMSUNG Tanzania wameanzisha mfumo wa kuweka stika mbili katika bidhaa
zao kwa ajili ya utambuzi wa bidhaa zao halisi pamoja na kupambana na bidhaa
feki nchini. Sambamba na mkakati huo Samsung piawameanzisha Kampeni ya ‘Nunua
Sajili na Ushinde’.
Kampenihiyo ya mwezi mzima inayolenga kutokomeza bidhaa
feki nchini itaanza tarehe 16 ya mwezi juni katika mikoa yote ya Tanzania, na itaambatana na promosheni
kabambe inayotarajiwa kuwazawadia
mamilioni ya watanzania watakao nunua
bidhaa halisi za Samsungkama vile TV, Friji, Microwave, mashine ya kufulia
pamoja na Viyoyozi.
“Ukizingatia bidhaa feki zina
hatarisha afya za watumiaji, mahitaji ya bidhaa bora na halisi yanaongezeka kwa
kasi kila kukicha. Samsung tumeendelea kufanya jitihada zaidi katika kukidhi
matakwa ya wateja wetu ulimwenguni pamoja
na Tanzania kwa ujumla. Samsung Tanzania inaamini kwamba kampeni ya ‘Nunua,
Sajili, Na Ushinde’ itaongeza uzoefu mpya na uelewa kwa wateja wetu wa dar es salaam na mikoani pia
juu ya utambuzi wa bidhaa feki zisizo kuwa za Samsung” alisema Meneja Bidhaa
kutoka Samsung, Elias Mushi.
Akiongeleakuhusumkakati huo mpya Bw Mushi alisema ‘tumeongeza alama mpya
kwenye bidhaa zetu ambazo ni stika mbili zitakazo wasaidia wateja kutambua
bidhaa feki sokoni, Bidhaa za Samsung zitakuwa na stika mbili, stika msambazaji
na stika inayotambulisha bidhaa halisi ya Samsung. Kampeni ya ‘Nunua Sajili na
Ushinde’ itakua ni kiunganishi cha kupeleka elimu kwa wateja wetu ambayo
itawapa taarifa za bidhaa zetu zinazoenda sambamba na mahitaji ya matumizi yao.
Pamoja na kampeni hiyo kabambe Samsung wataendesha bahati nasibu ambayo
washindi watajinyakulia zawadi kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Wateja wa
Samsung watafaidika na mpango huu kwa kusajili namba za bidhaa zao mara tu
wanaponunua bidhaa hiyo. Hii itafanyika kwa kutuma namba ya bidhaa kwenda namba
0798222333. Wateja watapata meseji ya uthibitisho wa bidhaa halisi ya Samsung
papo hapo. Kwa kufanya hivo Mteja atakuwa amejiunga moja kwa moja kwenye droo
ambayo itamwezesha kuwa mshindi wa bidhaa bora za Samsung zinakuja na waranti
ya miezi 12.
Kusherehekea uzinduzi huo wa Nunua Sajili na Ushinde pamoja na kusambaza elimu
juu ya stika hizo mbili kwa watanzania Samsung inaendesha kampeni ya
uhamasishaji nchi nzima kwa kipindi cha mwez mmoja.
Kwa kupitia mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika makao makuu ya
Samsung. Samsung wametangaza kuingia ubia wa usambazaji na kampuni ya Tanzania
Pyramid Consurmers ltd. Makubaliano yamehusisha usambazaji wa bidhaa mpya na za
kisasa za kieletroniki za Samsung. Makubaliano hayo yatapelekea makampuni hayo
mawili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa bora na halisi za Samsung ndani ya
Tanzania.
Bidhaa za Samsung ambazo zinasambazwa mpaka sasa na Tanzania Pyramid Consumers
ltd, ni pamoja na tv, friji, viyoyozi, mashine za kufulia pamoja na microwave.
Akifafanua kuhusu makubaliano hayo Bw Mushi alisema “tunafuraha kuungana
na Tanzania pyramid consumers ltd kwenye usambazaj wa bidhaa zetu. Tupo mbioni kutambulisha bidhaa
zetu mpya na pia tumejipanga kuongeza uwepo wetu nchi nzima kwa ajili ya
kurahisisha upatikanaji wa bidhaa bora na halisi za Samsung nchini” akaongeza kuwa “lengo letu ni kuendelea
kuboresha huduma kwa wateja wetu kila Nyanja pamoja na kutanua wigo mpana wa
mauzo pamoja na kuwafika wateja wetu maana wao ndo nguzo ya mafanikio yetu.
Muungano wetu na Pyramid Consurmers umetufanya tuwafikie wateja wetu kwa
urahisi, kwa haraka na kwa kuwapa mahitaji sahihi kwa kile wanachohitaji”
Karen Babu Meneja wa Pyramids consumers aliongezea kuwa “ Samsung ni
kampuni kubwa inayozidi kujitanua na
yenye ubunifu wa hali ya juu kwenye
bidhaa zake hivyo tunajivunia kutumia uzoefu wetu na ujuzi tulionao
kufanikisha malengo haya yote kwa pamoja. Pia tunajivunia kushirikiana na
Samsung kwa pamoja tutafanikisha kufikia soko la Tanzania kwa kiwango cha juu”
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment