Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
WATOTO watatu
ambao walipelekwa Marekani kwa ajili ya
matibabu zaidi mara baada ya kujeruhiwa katika ajali iliyotokea hivi
huko karatu na kuhusisha vifo 32 vya wanafunzi pamoja na
walimu hali zao zinaendelea vizuri.
Majeruhi wawili kati yao wakiwa
wamesharuhusiwa kutoka hospitalini na kupelekwa kituo maalum cha
uangalizi ambacho wauguzi na madaktari watakuwa wanawaangalia kwa saa
24 na baada ya hapo watatoa maamuzi ya kuwaruhusu kwenda nyumbani.
Aidha mtoto mmoja ambae ni Doreen aliefanyiwa upasuajia
maeneo mbali mbali kwenye mwili wake amebaki katika wodi ya watoto
katika hospitali ya Mercy kwa ajili ya kuendelea na matibabu ya karibu
zaidi ambapo baada ya madaktari kuridhika na afya yake nae
watamruhusu.
Hayo yalisemwa jana na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambae ni mmoja wa aliyefanikisha safari ya
majeruhi hao,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa
kuhusiana na jinsi ambavyo hali za watoto hao zinaendelea.
Alisema watoto wawili walioruhusiwa ni Sadia
na Wilson ndio walioruhusiwa kutoka hosptali na kupelekwa kwenye kituo maalum
cha uangalizi.
Alisema kuwa mtoto doreen amebaki kwenye wodi kutokana na
yeye kufanyiwa operesheni katika maeneo mengi ya mwili huku operesheni
yake ikiwa imechukua muda wa saa saba tofauti na wenzake na kwamba
mara baada ya madaktari kuridhika na uimara wake wa mfumo wa uti wa
mgongo ataruhusiwa kutoka kwenye hatua ya kwanza na kwenda hatua ya
pili ambapo hadi sasa hali yake nae inaendelea vizuri.
Nyalandu alidai kuwa yeye kama mtanzania aliyeguswa na
ajali hiyo anazidi kuwashukuru sana watanzania wote kwa kuungana kwa
pamoja kuwaombea watoto hao kwani Mungu amewaponya na anaamini watarejea
tena ili kuweza kuendelea na masomo yao .
"Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana watanzania
waliowaombea watoto hawa kwani matumaini makubwa yameonekana sana kwani
naamini hatua waliyotoka hawa watoto ni kubwa sana na naamini baada ya
kutoka hatua hii ya pili ya kuwa kwenye kituo maalum cha uangalizi
wataruhiswa kwenda majumbani"aliongeza Nyalandu.
Aidha aliishukuru serikali kwa jitiada zote iliyofanya ya
kuungana kwa pamoja kuwasafirisha watoto hao hadi Marekani ikiwa ni
pamoja na kuwashukuru waliotoa ndege za kuwasafirisha pamoja na
madaktari na wauguzi wa hopitali ya mount meru ambao wamejitolea
kuhudumia watoto.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment