Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 28 June 2017

MWANZA BINGWA UMITASHUMTA



 Viongozi na wachezaji wa timu ya UMITASHUMTA Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka mabingwa wa michezo hiyo kitaifa mwaka huu 2017.



 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela pamoja na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza.



Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela pamoja na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako wakifungua shampeni huku wakiipongeza mkoa wa Mwanza
                                                                        ********************
Na Alexander Sanga,Mwanza
Mkoa wa Mwanza umeiibuka bingwa wa jumla katika mashindano ya michezo ya shule ya msingi nchini kwa mwaka 2017

Mwanza imetwa ubingwa huo katika michezo hiyo iliyokuwa ikifanyika katika shule ya msingi ya Butimba na chuo cha ualimu cha Butimba TTC mjini hapa

Katika riadha upande wa wasichana  mkoa wa Manyara ulishika nafasi ya Tatu,Simiyu ikawa ya pili na Mwanza ilikuwa ya Kwanza.Upande wa riadha wavulana mkoa wa Geita iliibuka na ushindi nafasi ya pili ilichukuliwa na Shinyanga na mkoa wa Manyara uliambulia nafasi ya tatu.

Katika kombe la usafi upande wa wavulana, Dodoma ilikuwa ya kwanza ikifuatiwa na  Songwe kisha Mbeya ikiwa ya Tatu.

Kwa wasichana  Manyara ilikuwa ya kwanza huku Dodoma ilimaliza katika nafasi ya pili na  Kilmanjaro ikamaliza nafasi ya Tatu.

Kwenye mchezo wa Mpira wa wavu kwa wavulana mkoa wa Dar-es-salaam ulitwa ubingwa,Mwanza ilimaliza nafasi ya pili na Katavi ikawa nafasi ya Tatu.Upande wa wasichana Katavi ilitwa ubingwa na nafasi ya pili ilichukuliwa na Mtwara huku Geita ilimaliza nafasi ya Tatu.

Katika mchezo wa mpira wa mikono,kwa wavulana Songwe ilitwa ubingwa,Mwanza ikamaliza nafasi ya pili na Geita ilikuwa ya Tatu.kwa upande wa wasichana Mwanza ilitwaa ubingwa,Geita ikawa ya pili na mara ilishika nafasi ya Tatu.

Katika soka maalumu kwa wavulana Njombe ilitwaa ubingwa,Kagera ilishika nafasi ya pili na Dar-es-salaam iliambulia nafasi ya tatu.

Katika soka la kawaida wavulana,Mwanza ilitwaa ubingwa,Morogoro iliambulia nafasi ya pili na Mara ikawa nafasi ya Tatu.

Katika mchezo wa netiboli,Mwanza ilitwaa ubingwa,Geita ilishika nafasi ya pili na Arusha waliambulia nafasi ya Tatu.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce Ndalichako alisema serikali itaendelea kuinua vipaji katika michezo na aliziomba Halmashauri zitenge bajeti maalumu kwajili ya michezo


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment