Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 24 June 2017

MAKAMU WA RAIS AZITAKA KAMPUNI ZA MAFUTA NA GESI NCHINI KUTUMIA BIDHAA NA HUDUMA ZINAZOPATIKANA NCHINI

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka kampuni zilizowekeza katika sekta ya mafuta na gesi nchini kuhakikisha zinanunua huduma na bidhaa zinazopatikana nchini. Anaandika Katuma Masamba.

Amesema hitaji la watoa huduma wa Kitanzania kunufaika linaendana na sheria ya mafuta ya mwaka 2015 inayosisitiza katika ununuzi wa bidhaa na huduma zinazopatikana ndani.

Samia ameyasema hayo wakati akizundua Jumuiya ya Watoa Huduma Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jijini Dar es Salaam ambapo pia alipongeza uanzishwaji wa jumuiya hiyo kwa kuwa una lengo sawa na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Na pale ambapo huduma na bidhaa hazipatikani nchini, basi makampuni hayo yanapaswa kununua kutoka kwenye makampuni ya ndani yenye wabia nje ya nchi,” amesema Samia.

Alifafanua kuwa sheria hiyo imezingatia maslahi ya wananchi ikitaka hisa za makampuni ya ndani kutopungua asilimia 25 na kwamba kwa kununua bidhaa na huduma kutoka ndani ya nchi, Watanzania wengi walioko vijijini watanufaika.

Nae Balozi Ombeni Sefue ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa ATOGS aliiomba Serikali kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza Sera na Sheria.

"Watoa huduma hawa wamejiunga katika jumuia hii wakiwa na matarajio kwamba Serikali itashirikia kwa karibu na ATOGS katika kushughulikia changamoto na vikwazo vya  kibiashara na pia kufungua fursa kwa wafanyabiashara waliopo Tanzania," alisema Balozi Sefue.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment