Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 11 March 2017

WALIOFUKUZWA CCM DODOMA NA KUPEWA ONYO KALI HAWA HAPA

Na Mroki Mroki
Katibu wa Halamashuri Kuu, Itikadi na Uenezi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Humprey Polepole (pichani) amezungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita  katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Dodoma na kutoa taarifa ya Kikao cha Halamashauri Kuu ya CCM (NEC) kilichoketi leo kimepitisha maamuzi dhidi ya viongozi waliopatikana na makosa ya maadili kinyume na katiba na kanuni za uongozi na maadili ya CCM.

WENYEVITI WA MIKOA waliofukuzwa Uanachama ni pamoja na Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.


WAJUMBE WA HALAMASHAURI KUU YA TAIFA waliofukuzwa uanachama ni Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Babati, Ally Khera Sumaye, Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, Mathias Manga.

Aidha Wajumbe wa NEC waliovuliwa nafasi zao za Ujumbe ni pamojana na Mjumbe wa NEC kutoka Wialaya ya Tunduru, Ajili Kalolo, Mjumbe wa NEC Wialaya ya Singida Mjini, Hassan Mazala na Mjumbe wa NEC Wilaya ya Kibaha Mjini, Valerian Burreta huku Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Kilwa, Ali Mchumo akipewa onyo kali.

WENYEVITI WA WILAYA waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha, Wilfred Ole Soilel Molel, Mwenyekiti wa Wialya ya Kinondoni, Salum Kondo Madenge, Mwenyekiti wa Wialaya ya Longido, Makolo Laizer, Mwenyekiti wa Wilaya ya Babati, Ally Msuya na Mwenyekiti wa Wilaya ya Gairo Omar Awadh.

Wenyeviti walioachishwa uongozi ni pamoja na Abeid Kiponza wa Wilaya ya Iringa mjini, Hamisi Nguli wa Wilaya ya Singida Mjini huku Mwenyekiti wa Wilaya ya Muleba Muhaji Bushako akipewa onyo kali.

VIONGOZI WA JUMUIA ZA CCM ambao wamekubwa na adhabu ni pamoja na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake (UWT) Taifa na Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama wa CCM.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma na Mbunge wa Viti Maalum, Josephine Gezabuke amepewa onyo kali.

MJUMBE WA KAMATI KUU ambaye nae amekubwa na adhabu ni Balozi Emmanuel Nchimbi ambaye amepewa Onyo kali na kutakiwa kuomba radhi huku Mjumbe mwingine ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akisamehewa.

Kutokana na adhabu hizo walizopewa wanachama akiwepo Mbunge Sophia Simba anakosa sifa ya kuendelea kuwa mwanachama huku wale walio pewa maonyo makali wakitakiwa kutogombea nafasi zozote ndani ya chama kwa kipindi cha miaka minne.
    
CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia Simba, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment