Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu
ya INUKA ESTA iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Wanawake na Watoto ya KKKT
Dayosisi ya Konde.
Mkurugenzi
wa Wanawake na Watoto KKKT Dayosisi ya Konde, Alice Mtui akisoma risala
ya Uzinduzi wa Programu ya Inuka Esta mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Amos Makalla Askofu
Mstaafu wa Kanisa la Anglican, John Mwela akitoa neno katika uzinduzi
wa Programu ya INUKA ESTA iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Wanawake KKKT
Dayosisi ya Konde Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipokea zawadi ya Keki kutoka kwa viongozi wa Kurugenzi wa Wanawake Baadhi ya Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya baada ya kumaliza uzinduzi wa Programu ya INUKA ESTA
Wanawake wa Kikristo wakiwa katika ukumbi wa Tughimbe wakifuatilia uzinduzi wa programu ya Inuka Esta
*******************
KURUGENZI ya Wanawake na Watoto ya Kanisa la Kiinjili Kilutheli
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde imeshangazwa na uwepo wa utapiamlo na
udumavu wa Watoto licha ya Mkoa wa Mbeya kuongoza katika uzalishaji wa
mazao ya Chakula.
Kurugenzi hiyo ilibainisha kushangazwa huko katika Risala iliyosomwa
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati wa uzinduzi wa
Programu za Wanawake ziitwazo INUKA ESTA.
Akisoma Risala hiyo, Mkurugenzi wa Wanawake na Watoto KKKT Dayosisi
ya Konde, Alice Mtui alisema lengo la kuzindua Programu hiyo ambayo
itabeba vipindi mbali mbali vya kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuwainua
Wanawake wa KKKT na kuwavuta wasio wakristo kuvaa uhusika wao,
Alisema lengo lingine ni kuhamasisha wanawake wa Jukwaa la kikristo
Mbeya ili kuleta ukombozi kwenye maisha ya familia na jamii na
kurejesha hadhi na thamani ya utu pamoja na maadili yanayozidi kushuka
na kuporomoka katika kizazi cha sasa.
Kuhusu uwepo wa Utapiamlo katika jamii, Mkurugenzi huyo alisema ni
jambo la aibu kwa Mkoa wa Mbeya ambao ni kati ya mikoa mikubwa mitano
inayolisha Nchi lakini ni Mkoa wenye Utapiamlo na udumavu wa akili kwa
watoto.
“Sio kweli kwamba watu wa Mbeya hawawezi kulisha familia zao chakula
kipo cha kutosha na WanaMbeya wanauwezo mkubwa wa kulisha familia zao
lakini tatizo kubwa ni wazazi na walezi wengi hawako makini kufuatilia
na kupangilia lishe katika familia zao” alisema Mtui.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema Mkoa wa
Mbeya unaongoza kwa kuwa na makanisa mengi lakini baadhi ya dini zinatoa
doa kwa Mkoa kutokana na matendo maovu yanayotokea kila siku.
Alisema baadhi ya dini zinahamasisha waumini wao kufukua makaburi ili
wawaombee marehemu na kuwafufua jambo ambalo haliwezekani, matendo ya
kuzika watu wakiwa hai na wengine kuzuia watu kuzikwa baada ya kufariki.
Aidha alitoa wito kwa Wanawake kusaidia kukemea maovu katika jamii
hususani uuzaji na unywaji wa pombe zilizopigwa marufuku kama viloba na
kilimo cha Bhangi na matumizi ya dawa za kulevya.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment