Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 27 February 2017

BAADA YA MIAKA 53 HATIMAYE WANANCHI WA MTAA WA IGUNGANDEMBWE MANISPAA YA IRINGA WAPATA MAJI SAFI NA SALAMA

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye aliyechimba kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
 Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.
 
Wakizungumza na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.

“Angalia maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.

Wananchi wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.

Kabati alisema kuwa ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.

“Hivi  hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema Kabati

Aidha Kabati alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi ya Rais wetu.

Naye Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo na kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili kuendelea kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.

Mtove aliongeza kuwa atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata hiyo.

“Angalia hadi saizi tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na changamoto nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa na vikwazo vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.


Sunday 26 February 2017

MSIKIE MSAMARIA MWEMA WA NEEMA WAMBURA AKIELEZEA NAMNA RAIS MAGUFULI ALIVYOWAPIGIA SIMU


Saturday 25 February 2017

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA IKULU DAR ES SALAAM LEO


RAIS MUSEVENI AWASILI NCHINI NA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS MAGUFULI



Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amewasili hapa nchini leo kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Museveni amepokelewa na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Tanzania Bara na Zanzibar wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Akiwa Uwanjani hapo Mhe. Rais Museveni amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 iliyokwenda sambamba na nyimbo za mataifa yote mawili na wimbo Jumuiya ya Afrika Mashariki na kisha akakagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye akashuhudia burudani ya vikundi vya ngoma na matarumbeta. 

Baada ya mapokezi hayo rasmi, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na mgeni wake Mhe. Rais Museveni Ikulu Jijini Dar es Salaam na baadaye viongozi wote wawili wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari.

Katika hotuba yake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Museveni kwa kukubali mwaliko wake wa kuitembelea Tanzania na kueleza kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendeleza ushirikiano na uhusiano wa kidugu uliopo kati ya Tanzania na Uganda huku akitilia msisitizo wa uhusiano huo kujikita katika kuongeza biashara na kuharakisha miradi ya maendeleo inayoziunganisha nchi hizi mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema japo kuwa biashara kati ya Tanzania na Uganda imekua kutoka Shilingi Bilioni 178.19 mwaka 2015 hadi kufikia Shilingi Bilioni 193.59 mwaka 2016 bado nchi hizi zinapaswa kuongeza zaidi na ametoa wito kwa wafanyabiashara wa nchi zote mbili kushirikiana zaidi katika biashara na uwekezaji.

“Uwekezaji wa wafanyabiashara wa Uganda hapa nchini Tanzania una thamani ya Dola za Marekani Milioni 46.05 na umezalisha ajira 1,447”

“Watanzania wanaoishi Uganda ni wengi kuliko wanaoishi katika nchi nyingine yoyote duniani, hii ina maana tunapaswa kushirikiana zaidi na kufanya biashara zaidi” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema ili kukuza biashara na Uganda, Tanzania imeanza kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo kujenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambayo itakwenda pamoja na ujenzi wa bandari kavu Mkoani Mwanza ili wafanyabiashara wa Uganda wasilazimike kuja mpaka bandari ya Dar es Salaam kuchukua mizigo yao inayotoka nje ya nchi kwa meli, kukarabati meli ya MV Umoja itakayovusha mizigo mpaka bandari ya Port Bell kupitia ziwa Viktoria, kununua ndege 6 za kusafirisha kwa ajili ya Shirika la ndege la Taifa (ATCL) na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kufikia 3.

Kuhusu mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania ipo tayari ujenzi huo uanze baada ya kukamilisha mazungumzo ya masuala machache yaliyokuwa yamebaki na ametaka wawekezaji waanze kazi ya ujenzi badala ya kuleta visingizio.

Kwa upande wake Mhe. Rais Museveni amemshukuru Rais Magufuli kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na amesema Uganda itaendelea kuwa ndugu na rafiki wa kweli wa Tanzania huku akisisitiza kuwa rafiki na ndugu wa kweli ni lazima wawe wamoja katika maamuzi na mipango mbalimbali ikiwemo maendeleo na biashara.

Mhe. Rais Museveni amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kufuata nyayo za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokana na juhudi zake za kujenga reli ya kati, kununua ndege, kufufua biashara kati ya Tanzania na Uganda na msimamo wake kuukataa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya ambao umeoneka kutokuwa na manufaa ya kiuchumi kwa Afrika Mashariki ikiwemo kutishia mpango wa ujenzi wa viwanda.

“Nimefurahi kuwa Mhe. Magufuli unafuata nyayo za Mwalimu Nyerere, mimi pia ni mfuasi wa Mwalimu Nyerere, hata nilipokuja Tanzania kusoma nilikuwa namfuata Mwalimu Nyerere” amesema Mhe. Rais Museveni.

Mhe. Rais Museveni ametoa wito kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima kuzungumza lugha moja na ziwe na msimamo wa pamoja ili kukabiliana na ukoloni ambao huko nyuma ulitawala kutokana na watawala wa Afrika kukosa umoja.

Kuhusu bomba la Mafuta, Rais Museveni amesema atafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo hasa baada ya uamuzi kufanyika kuwa bomba la mafuta yaliyogundulika Hoima nchini Uganda litapitia Tanzania hadi bandari ya Tanga.

Jioni hii Mhe. Rais Museveni atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.


BALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS

 Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais François Hollande wa Ufaransa mjini Paris.


MBUNGE RITTA KABATI KUSAIDIA UJENZI WA OFISI TATU ZA CHAMA CHA MAPINDUZI MANISPAA YA IRINGA

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akimkabidhi mifuko ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama katika kata ya Ruaha kwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa katika eneo la uwanja wa kujenga ofisi ya kata ya Ruaha
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akibadilishana mawazo na katibu wa ccm manispaa ya Iringa Nuru Ngereja
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa hama hicho wa kata ya ruaha
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akipokelewa na wanachama wa mtaa wa kigamboni mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameanza kusaidia Ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM katika kata mbali mbali za Jimbo la Iringa mjini kama sehemu ya majukumu yake ya kukijenga chama hicho ambacho kilipoteza kiti cha ubunge na halmashauri kuchukuliwa na wapinzani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi Kigamboni na Ruaha ,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio ya miaka arobaini ya chama cha mapinduzi.
“Nakipenda chama changu ndio maana napigana sana kuhakikisha chama cha mapinduzi mkaoni mhapa iringa kinarudi mahala pake na kuhakikisha kinaaminika kwa wananchi na wanachama wa  manispaa ya Iringa”.alisema Kabati 

Hata hivyo Kabati alisema kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi linakuwa na ofisi yake ya tawi na aliwataka wanachama wa CCM kushikamana na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na kujihusisha na shughuli nyingine za kijamii

"Haiwezakani chama kikubwa kama hiki kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi ya kujenga ofisi nitakikisha tunashirikiana na wanachama na wananchi wengine kujenga hizo ofisi ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli ambaye anapambana kuhakikisha cha mapinduzi kinakuwa chama cha wananchi wa chini na sio matajiri pekee yao".alisema Kabati

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza aliwataka wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza kujenga chama upya.
“Tulipoteza halmashauri ya Iringa na jimbo hivyo inabidi tukae chini na tujipange upya kukijenga chama maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi zitatusaidia kurudisha hadhi na hali ya chama hapa manispaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua chama”.alisema Kiponza 

Kiponza alimshukuru mbunge wa viti maalumu Ritta kabati kwa mchango anaoutoa kwa kuleta maendeleo katika manispaa ya Iringa hasa ukiangalia ujenzi wa majengo mbalimbali ya shule,taasisi za kidini,taasisi za kijamii hapa kujenga majengo ya chama.

Lakini Kiponza alimtaka mbunge Kabati kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika manispaa ya Iringa.

“Hapa kigamboni kunawananchi wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM tu na wamenyang’anywa kituo cha kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa chama cha mapinduzi hivyo lazima upambane kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na mali za chama zinarudi kwenye chama”.alisema Kiponza

 Naye Katibu wa CCM manispaa ya Iringa Nuru Ngeleja alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha ofisi zote za chama zinajengwa na zinakuwa katika ubora unaotakiwa kutokana na ukubwa wa chama cha mapinduzi(CCM) na kuahidi kuwa wataendelea kumuunga mkoano Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr John Pombe Magufuri.

“Sisi tunafanyakazi ya kumsaidia mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais wetu kwa kufanya kazi na kuisimamia serikali kufanya kazi kwa uhakika na kuwafaikia na kuwatumikia wananchi waliowaweka madarakani mpaka sasa”. Alisema Ngereja