Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.Nafasi Ya Matangazo

Friday, 7 April 2017

KOMBE LA DUNIA 2018 MUBASHARA DSTVSuperSport imethibitisha kuwa ni kitovu cha burudani hususan ya soka baada ya kukamilisha makubaliano makubwa na shirikisho la soka la dunia FIFA ikiwemo kurusha kombe la dunia mwaka 2018 mubashara. Michuano hiyo itafanyika nchini Urusi

Burudani ya  soka kwa wateja wote wa DStv itakuwa ya aina yake kwani mechi zote 64 zitaonyeshwa mubashara kwenye mgumo wa High Definition, hii ikimaanisha kuwa wateja wa DStv watauona mtanange huo katika muonekano bora zaidi.

Makubaliano mengine yaliyofikiwa kati ya SuperSport na FIFA ni pamoja na urushwaji wa matangazo ya Kombe la dunia la timu za umri wa chini ya miaka 20 maarufu kama U-20 pamoja nay ale ya wachezaji wa wenye umri wa chini ya miaka 17 yaani U-17. Mashindano mengine ambayo yatarushwa na SuperSport ni pamoja na Kombe la dunia la soka la ufukweni  pamoja na kombe la dunia la U-20 na U17 kwa wanawake.

Makubaliano haya yanaendelea kuifanya SuperSport kuwa gwiji kwenye kutoa burudani hususan soka ukizingatia kuwa bado wanaendelea kurusha ligi maarufu duniani kama ile ya Uingereza , Hispania, Afrika Kusini na kadhalika.

“Kandanda ni lulu kwenye SuperSport” anasema Mkurugenzi Mkuu Gideon Khobane. “tumekuwa kukifurahia burudani ya kombe la dunia kwa miaka mingi na kwa makubaliano haya ya sasa tuna uhakika wa kuendelea kuwapa wateja wetu burudani zaidi. Cha msingi, wateja wetu wategemee burudani ya kiwango cha juu”.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment