Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 5 March 2017

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM KUTOKA KATIKA ZIARA YA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya kulevya nchini Bw. Rogers Sianga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017.

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017



Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017.   PICHA NA IKULU.
*******************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Machi, 2017 amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 4 katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Kabla ya kuondoka Mjini Mtwara na kurejea Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Magufuli amefanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mashujaa Mjini Mtwara ambapo amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha inasukuma maendeleo ya Mtwara na Lindi kwa nguvu kubwa kwa manufaa ya wananchi.

Amesema Serikali imedhamiria kutilia mkazo juhudi za uendelezaji wa bandari ya Mtwara, ujenzi wa barabara, uimarishaji wa miundombinu ya nishati ya umeme, ujenzi wa viwanda vikubwa na usimamizi mzuri wa shughuli za kilimo ambavyo vitasaidia kukuza uchumi, kuzalisha ajira na kuboresha maisha ya watu.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa mafanikio yaliyopatikana katika soko la korosho lililopita na ameagiza wale wote waliohusika kufuja fedha za wakulima wachukuliwe hatua.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amesema Tanzania itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake mzuri na nchi jirani ya Msumbiji na ametaka suala la wahamiaji haramu wanaoondolewa nchini humo wakiwemo Watanzania lisikuzwe huku akisisitiza kuwa Serikali haiwezi kuwatetea watu wanaishi katika nchi nyingine bila kufuata sheria.

Kuhusu Mkoa wa Mtwara kufanya vibaya kielimu, Mhe. Rais Magufuli amewataka wananchi wa Mtwara kubadilika kwani juhudi za Serikali kuwapelekea maendeleo hazitakuwa na maana kama wananchi watakuwa hawana elimu.

"Nimeambiwa hapa watu wanapenda sana disco na ngoma, watoto badala ya kusoma wanacheza disco, hapo tunakwenda pabaya" amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mkutano wa Mhe. Rais Magufuli Mjini Mtwara umedhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, Wabunge na viongozi wa taasisi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment